YouVersion Logo
Search Icon

Zab 87

87
Shangwe ya Kuishi Sayuni
Ya Wakorahi. Zaburi. Wimbo.
1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3 # Isa 60:1 Umetajwa kwa mambo matukufu,
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;
Huyu alizaliwa humo.
5 # Eze 48:35; Mt 16:18 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye juu
Ataufanya imara.
6 # Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9 BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.

Currently Selected:

Zab 87: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in