YouVersion Logo
Search Icon

Zab 85

85
Sala ya Kupata Fadhili za Mungu Tena
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.
1 # Yer 30:18; Eze 39:25 BWANA, umeiridhia nchi yako,
Umewarejeza mateka wa Yakobo.
2Umeusamehe uovu wa watu wako,
Umezisitiri hatia zao zote.
3Umeiondoa ghadhabu yako yote,
Umerudi na kuuacha ukali wa hasira yako.
4Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,
Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
5Je! Utatufanyia hasira hata milele?
Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi?
6 # Hab 3:2 Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha,
Watu wako wakufurahie?
7Ee BWANA, utuonyeshe rehema zako,
Utupe wokovu wako.
8 # Hab 2:1; Zek 9:10; 2 Pet 2:20 Na nisikie atakavyosema Mungu BWANA,
Maana atawaambia watu wake amani,
Naam, na watauwa wake pia,
Bali wasiurudie upumbavu tena.
9Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.
10 # Mik 7:20; Yn 1:17; Zab 72:2,3; Isa 32:17; Lk 2:14; Yn 14:27 Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amani zimehusiana.
11 # Isa 45:8; 2 Kor 5:14-21 Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni.
12 # Yak 1:17 Naam, BWANA atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
13Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.

Currently Selected:

Zab 85: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in