YouVersion Logo
Search Icon

Zab 66

66
Sifa kwa Ajili ya Wema wa Mungu kwa Israeli
Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi.
1Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
2Imbeni utukufu wa jina lake,
Tukuzeni sifa zake.
3 # Zab 18:44 Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini!
Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako,
Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
4 # Zab 67:3 Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,
Naam, italiimbia jina lako.
5 # Zab 46:8 Njoni yatazameni matendo ya Mungu;
Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;
6 # Kut 14:21; Yos 3:14-17; Zab 78:13; Isa 63:13,14 Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;
Katika mto walivuka kwa miguu;
Huko ndiko mlikomfurahia.
7 # Zab 11:4 Atawala kwa uweza wake milele;
Macho yake yanaangalia mataifa;
Waasio wasijitukuze nafsi zao.
8Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,
Itangazeni sauti ya sifa zake;
9Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai,
Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.
10 # Zek 13:9 Kwa maana umetupima, Ee Mungu,
Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
11Ulituingiza ndani ya wavu,
Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
12Uliwapandisha watu
Juu ya vichwa vyetu.
Tulipita motoni na majini;
Ukatutoa na kutuleta kunako wingi.
13 # Zab 116:14,18; Mhu 5:4; Yon 2:9 Nitaingia nyumbani mwako na kafara;
Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
14Ambazo midomo yangu ilizinena;
Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.
15Kafara za vinono nitakutolea,
Pamoja na fukizo la kondoo waume,
Nitatoa ng’ombe pamoja na mbuzi.
16Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu,
Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
17Nalimwita kwa kinywa changu,
Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
18 # Ayu 11:14,15; Mit 15:29; Isa 1:15 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu,
Bwana asingesikia.
19Hakika Mungu amesikia;
Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.
20Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu,
Wala kuniondolea fadhili zake.

Currently Selected:

Zab 66: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in