YouVersion Logo
Search Icon

Zab 51

51
Sala ya Utakaso na Msamaha
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi, wakati Nabii Nathani alipomjia, alipokuwa amekwisha kwenda kwa Bathsheba
1 # Kol 2:14 Ee Mungu, unirehemu,
Sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
2 # Eze 36:25; Zek 13:1; 1 Kor 6:11; Ebr 9:14; 1 Yoh 1:7; Ufu 1:5 Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu.
3 # Zab 32:5 Maana nimejua mimi makosa yangu
Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
4 # Rum 3:4; Lk 15:21; Mwa 39:9 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,
Na kufanya maovu mbele za macho yako.
Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,
Na kuwa safi utoapo hukumu.
5 # Ayu 14:4; Yn 3:6; Rum 5:12 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;
Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;
Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,
Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8Unifanye kusikia furaha na shangwe,
Mifupa uliyoiponda ifurahi.
9Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;
Uzifute hatia zangu zote.
10 # Mit 20:9; Yer 13:27; Eze 11:19; Mdo 15:9; Efe 2:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
11 # Mwa 4:14; Eze 36:27; Rum 8:9 Usinitenge na uso wako,
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12 # Rum 8:15; 2 Kor 3:17 Unirudishie furaha ya wokovu wako;
Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
13Nitawafundisha wakosaji njia zako,
Na wenye dhambi watarejea kwako.
14Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,
Uniponye na damu za watu,
Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
15Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,
Na kinywa changu kitazinena sifa zako.
16Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
17Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka,
Ee Mungu, hutaudharau.
18Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,
Uzijenge kuta za Yerusalemu.
19 # Mal 3:3 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,
Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.
Ndipo watakapotoa ng’ombe
Juu ya madhabahu yako.

Currently Selected:

Zab 51: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy