YouVersion Logo
Search Icon

Zab 31

31
Sala na Sifa kwa Kukombolewa kutoka kwa Adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Nimekukimbilia Wewe, BWANA,
Nisiaibike milele.
Kwa haki yako uniponye,
2 # Zab 71:2; Mit 22:17 Unitegee sikio lako, uniokoe hima.
Uwe kwangu mwamba wa nguvu,
Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
3 # Zab 23:3; Yer 14:7 Ndiwe genge langu na ngome yangu;
Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
4Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,
Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
5 # Lk 23:46; Mdo 7:59; 2 Tim 1:12; Ebr 6:18 Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.
6Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo;
Bali mimi namtumaini BWANA.
7 # Yn 10:27 Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako,
Kwa kuwa umeyaona mateso yangu.
Umeijua nafsi yangu taabuni,
8 # Zab 18:19 Wala hukunitia mikononi mwa adui;
Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.
9Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki,
Jicho langu limenyauka kwa masumbufu,
Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
10Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni,
Na miaka yangu kwa kuugua.
Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu,
Na mifupa yangu imekauka.
11 # Zab 88:8 Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu,
Naam, hasa kwa jirani zangu;
Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu;
Walioniona njiani walinikimbia.
12Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa;
Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.
13 # Yer 20:3; Omb 2:22; Mt 27:1 Maana nimesikia masingizio ya wengi;
Hofu ziko pande zote.
Waliposhauriana juu yangu,
Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
14Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA,
Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
15Nyakati zangu zimo mikononi mwako;
Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.
16 # Hes 6:25; Zab 4:6; Dan 9:17 Umwangaze mtumishi wako
Kwa nuru ya uso wako;
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
17 # Zab 25:2 Ee BWANA, nisiaibishwe, maana nimekuita;
Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.
18 # Zab 12:3 Midomo ya uongo iwe na ububu,
Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi,
Kwa majivuno na dharau.
19 # Isa 64:4; 1 Kor 2:9 Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako
Ulizowawekea wakuchao;
Ulizowatendea wakukimbiliao
Mbele ya wanadamu!
20 # Zab 27:5; Ayu 5:21 Utawasitiri na fitina za watu
Katika sitara ya kuwapo kwako;
Utawaficha katika hema
Na mashindano ya ndimi.
21BWANA ahimidiwe; kwa maana amenitendea
Fadhili za ajabu katika mji wenye boma.
22Nami nalisema kwa haraka yangu,
Nimekatiliwa mbali na macho yako;
Lakini ulisikia sauti ya dua yangu
Wakati nilipokulilia.
23 # 1 Pet 1:5 Mpendeni BWANA,
Ninyi nyote mlio watauwa wake.
BWANA huwahifadhi waaminifu,
Humlipa atendaye kiburi malipo tele.
24Iweni hodari, mpige moyo konde,
Ninyi nyote mnaomngoja BWANA.

Currently Selected:

Zab 31: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy