YouVersion Logo
Search Icon

Mit 19

19
1 # Mit 28:6 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,
Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu.
2 # Hos 4:6; Yn 16:3; Rum 10:2 Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa;
Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.
3 # Zab 37:7 Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake;
Na moyo wake hununa juu ya BWANA.
4Utajiri huongeza rafiki wengi;
Bali maskini hutengwa na rafiki yake.
5 # Kut 23:1 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;
Wala asemaye uongo hataokoka.
6Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili;
Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu.
7Ndugu zote wa maskini humchukia;
Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye!
Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.
8Apataye hekima hujipenda nafsi yake;
Ashikaye ufahamu atapata mema.
9 # Dan 6:24 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;
Naye asemaye uongo ataangamia.
10 # Mhu 10:6 Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu;
Sembuse mtumwa awatawale wakuu.
11 # Mit 25:21; Mt 5:44; Rum 12:19; Efe 4:32 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake;
Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
12Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;
Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
13Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye;
Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.
14 # 2 Kor 12:14; Mit 18:22 Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
15Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;
Na nafsi yake mvivu itaona njaa.
16 # Lk 10:28; Rum 2:7 Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake;
Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
17 # Mit 14:21; Mhu 11:1; 2 Kor 9:6 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA;
Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
18Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini;
Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
19Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake,
Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena.
20Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,
Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.
21 # Mwa 37:19,20; Est 9:25; Mhu 7:29; Isa 14:26; Ebr 6:17 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu;
Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.
22Haja ya mwanadamu ni hisani yake;
Ni afadhali maskini kuliko mwongo.
23 # 1 Tim 4:8 Kumcha BWANA huelekea uhai;
Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.
24Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;
Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.
25Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara;
Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa.
26Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye,
Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.
27 # Mt 7:15; Mk 4:24; Yn 10:5; Efe 4:14; 1 Tim 4:6 Mwanangu, acha kusikia mafundisho,
Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.
28Shahidi asiyefaa kitu hudhihaki hukumu,
Na vinywa vya wasio haki humeza uovu.
29Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha;
Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu.

Currently Selected:

Mit 19: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy