YouVersion Logo
Search Icon

Hes UTANGULIZI

UTANGULIZI
Hesabu ni kitabu cha nne katika mfuatano wa vitabu vya Biblia. Jina Hesabu linatokana na sehemu mbili za kitabu hiki ambazo zinahusu sensa mbili zilizofanywa kwa ajili ya jeshi. Sensa ya kwanza ni kwa Waisraeli waliotoka Misri (1:1-2:32) na ya pili ni kwa kizazi kipya cha walioingia Nchi ya Ahadi (26:1-15).
Kitabu hiki kinasimulia jinsi Waisraeli walivyopangwa katika makundi kwa kuzunguka Hema Takatifu, walivyosafiri toka Sinai kuelekea Kadesh-barnea na jinsi walivyojaribu kuingia katika Nchi ya Ahadi kutokea kusini lakini bila kufaulu. Aidha kuna masimulizi kuhusu imani, matumaini na moyo wa ushujaa kadhalika kutokuwa na imani, kukata tamaa, mashaka, woga na manung’uniko. Mungu ni mwaminifu kwa Agano na mwenye rehema. Masimulizi ya matukio ya kipindi chao cha kukaa jangwani miaka 38 wakijitayarisha na mwishoni walivyofanikiwa kutwaa sehemu za kusini mwa Mto Yordani na kuingia katika nchi waliyoahidiwa yana sehemu kubwa katika kitabu hiki.
Yaliyomo:
1. Sensa ya kwanza na kazi ya Walawi, Sura 1–4
2. Sheria na maongozi, Sura 5–8
3. Pasaka ya pili na safari toka Sinai, Sura, 9–10
4. Uasi jangwani na sheria mbalimbali, Sura 11–19
5. Safari toka Kadeshi hadi Moabu, Sura 20–25
6. Sensa ya pili na sheria kuhusu urithi, kafara na viapo, Sura 26–30
7. Katika Midiani na kugawana nchi, Sura 31–36

Currently Selected:

Hes UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in