YouVersion Logo
Search Icon

Hes 19

19
Kafara ya Ng’ombe Jike Mwekundu
1BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2#Isa 53:4-6; Gal 4:4; Ebr 9:13,14; Ufu 1:5; Kum 21:3; 1 Sam 6:7; Yn 10:17; Flp 2:6,8Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado; 3#Law 4:12,21; 13:46; 16:27; 24:14; Ebr 13:11nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye atakwenda naye nje ya kambi, na mtu mmoja atamchinja mbele yake; 4#Law 4:6,17; 16:14; Isa 52:15; Eze 36:25; Ebr 9:13,14; 12:24; 1 Pet 1:2kisha Eleazari kuhani atatwaa katika damu yake kwa kidole chake, na kuinyunyiza damu yake kuelekea upande wa mbele wa hema ya kukutania mara saba; 5#Kut 29:14; Law 4:11,12; Isa 53:10kisha mtu mmoja atamchoma moto huyo ng’ombe mbele yake; ngozi yake, na nyama yake, na damu yake, pamoja na mavi yake pia atachoma moto; 6#Law 14:4,6kisha kuhani atatwaa mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, na kuvitupa katika huo moto unaomchoma ng’ombe. 7#Law 11:25; 15:5Ndipo kuhani atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, kisha baadaye ataingia kambini, naye kuhani atakuwa najisi hata jioni. 8Na huyo aliyemchoma moto ng’ombe atazifua nguo zake majini, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hata jioni. 9#Ebr 9:13; Hes 31:23; Zek 13:1; 2 Kor 7:1Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng’ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi. 10Na yeye ayazoaye majivu ya huyo ng’ombe atazifua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; na jambo hili litakuwa amri ya milele, kwa wana wa Israeli, na wa mgeni akaaye kati yao. 11#Law 21:1; Hes 5:2; Isa 52:11; Rum 5:12; 2 Kor 6:17; Efe 2:1Mtu agusaye maiti ye yote atakuwa najisi muda wa siku saba; 12#Hes 31:19naye atajitakasa kwa yale maji siku ya tatu, na siku ya saba atakuwa safi; lakini kama hajitakasi siku ya tatu, ndipo na siku ya saba hatakuwa safi. 13#Law 15:31; Hes 8:7; Law 7:20; 22:3Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado. 14Hii ndiyo amri, mtu afapo ndani ya hema; kila mtu aingiaye ndani ya hema hiyo, na kila mtu aliye humo hemani, atakuwa najisi muda wa siku saba. 15#Hes 31:20; Law 11:32Na kila chombo kilicho wazi, kisichofungwa na kifuniko, ni najisi. 16Kisha mtu ye yote huko nje shambani atakayemgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga, au mfupa wa mtu, au kaburi, atakuwa najisi muda wa siku saba. 17Na kwa huyo aliye najisi watatwaa katika majivu ya kuchomwa kwake hiyo sadaka ya dhambi, na maji ya mtoni yatachanganywa na majivu katika chombo; 18#Zab 51:7; Yn 15:2; 17:19; 1 Kor 1:30; Ebr 9:14kisha mtu mmoja aliye safi atatwaa hisopo, na kuitia katika hayo maji naye atayanyunyiza juu ya hema, na juu ya vyombo vyote, na juu ya watu waliokuwapo, na juu yake yeye aliyeugusa mfupa, au mtu aliyeuawa, au mzoga, au kaburi; 19#Law 14:9na yule aliye safi atamnyunyiza huyo aliye najisi siku ya tatu, na siku ya saba; na katika siku ya saba atamtakasa; naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa safi jioni. 20#Mwa 17:14; Mk 16:16; Mdo 13:39-41; Rum 2:4,5; Gal 3:10Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yu najisi. 21Nayo itakuwa amri ya sikuzote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hata jioni. 22#Hag 2:13Na kitu cho chote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hata jioni.

Currently Selected:

Hes 19: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in