YouVersion Logo
Search Icon

Hes 14

14
Watu Wanaasi
1Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. 2#Zab 106:25; Kum 28:68Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? 4#Neh 9:17; Mdo 7:39; Ebr 11:15Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri. 5Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya mkutano wa kusanyiko la wana wa Israeli. 6Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; 7wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. 8#Kum 10:15; 2 Sam 15:25; 1 Fal 10:9; Zab 22:8; Isa 62:4; Hes 13:27Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. 9#Ebr 3:16; Kum 9:7,23,24; Kum 20:3; Hes 24:8; Mwa 48:21; Kut 33:16; Kum 20:1; 2 Nya 15:2; Isa 41:10Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope. 10#Kut 17:4; 16:10; Law 9:23Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.
11 # Ebr 3:8; Zab 78:22; Yn 12:37 BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao. 12#Kut 32:10Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.
Musa Awaombea Watu kwa Mungu
13 # Kut 32:11-14; Eze 20:9 Basi Musa akamwambia BWANA, Ndipo Wamisri watasikia habari hiyo; kwa kuwa wewe uliwaleta watu hawa kwa uweza wako, kutoka kati yao; 14#Kut 15:14; Neh 9:12kisha watawaambia wenyeji wa nchi hii; wamesikia wao ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa; maana, wewe BWANA waonekana uso kwa uso, na wingu lako lasimama juu yao, kisha wewe watangulia mbele yao, katika nguzo ya wingu mchana, na katika nguzo ya moto usiku. 15Basi kama wewe ukiwaua watu hawa mfano wa mtu mmoja, ndipo mataifa yaliyosikia habari za sifa zako watakaponena na kusema, 16#Yos 7:9Ni kwa sababu yeye BWANA hakuweza kuwaleta watu hao kuwatia katika nchi aliyowaapia, kwa ajili ya hayo amewaua nyikani. 17Basi sasa nakusihi sana, uweza wa Bwana wangu na uwe mkuu, kama ulivyonena, uliposema, 18#Kut 20:5-6; 34:6-7; Kum 5:9-10; 7:9-10; Zab 103:8; 145:8; Yon 4:2; Kut 34:7BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne. 19Nakusihi, usamehe uovu wa watu hawa, kama ukuu wa rehema yako ulivyo, kama ulivyowasamehe watu hawa, tangu huko Misri hata hivi sasa. 20#Yak 5:16; 1 Yoh 5:14BWANA akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa; 21#Ebr 3:18; Zab 72:19; Isa 5:16; 11:9; 61:11; Eze 18:3; Hab 2:14; Ufu 11:15lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA; 22#Kum 1:31,34; Zab 95:11; Ebr 4:6,7; Mwa 31:7kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu; 23#Kum 1:35; Zab 106:26; Eze 20:15; Ebr 3:18; 4:3hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona; 24#Yos 14:9-12; Zab 25:13; Isa 33:15; Mt 5:5lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki. 25Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu.
Ukaidi wa Waisraeli na Kushindwa Kwao
26Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 27#Kut 16:28; Mt 17:17; Mk 9:19; Kut 16:12; 1 Kor 10:10Je! Nichukuane na mkutano mwovu huu uninung’unikiao hata lini? Nimesikia manung’uniko ya wana wa Israeli, waninung’unikiayo. 28#Ebr 3:17Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi; 29#Hes 26:64mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung’unikia, 30#Kum 1:36,38hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliinua mkono wangu ya kwamba nitawaketisha humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. 31#Zab 106:24; Mit 1:25,26; Ebr 12:16,17Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi ninyi mliyoikataa. 32#1 Kor 10:5Lakini katika habari zenu, mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili. 33#Mdo 7:36; Zab 107:40; Kum 2:14Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hata mizoga yenu itakapoangamia jangwani. 34#Hes 13:25; Zab 95:10; Eze 4:6; 1 Fal 8:56; Zab 77:8; Ebr 4:1Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu. 35#Hes 23:19Mimi BWANA nimekwisha nena, hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote, waliokusanyika juu yangu; wataangamia katika nyika hii, nako ndiko Watakakokufa. 36#Hes 13:31Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung’unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi, 37#Yer 28:16,17; 1 Kor 10:10; Ebr 3:17; Yud 1:5watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA. 38#Yos 14:6Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.
39 # Mit 19:3; Mt 8:12; Ebr 12:17 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaombolea sana. 40#Kum 1:41; Mhu 9:3; Mt 7:21; Lk 13:25Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi. 41#2 Nya 24:20; Ayu 9:4; Isa 59:1,2; Yer 2:37; 1 Kor 10:22Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyahalifu maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo. 42#Kum 1:42; Zab 44:1-3Msikwee, kwa kuwa BWANA hamo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu. 43#Kum 1:43,44; Amu 16:20Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimwandame BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi. 44Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la agano la BWANA halikutoka humo maragoni, wala Musa hakutoka. 45Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakatelemka, wakawapiga na kuwaangusha, hata kufikilia Horma.

Currently Selected:

Hes 14: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy