YouVersion Logo
Search Icon

Hes 10

10
Baragumu za Fedha
1Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, 2#Zab 81:3; 89:15; Isa 1:13; Hos 8:1; Yoe 1:14Jifanyie tarumbeta mbili za fedha; utazifanya za kazi ya ufuzi; nawe utazitumia kwa kuwaita mkutano wakutane, na kwa kusafiri kwao yale makambi. 3#Yer 4:5; Yoe 2:15; Zab 22:22; 35:18; Isa 55:1-4; Zek 8:21-23; Ufu 22:17Na hapo watakapozipiga hizo tarumbeta, mkutano wote utakukutanikia wewe, hapo mlangoni pa hema ya kukutania. 4#Hes 1:16; 7:2; Kut 18:21Nao wakipiga tarumbeta moja tu ndipo wakuu, walio vichwa vya maelfu ya Israeli, watakukutanikia wewe 5#Hes 2:3Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha sana, marago yaliyoko upande wa mashariki yatasafiri. Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha ya pili, marago yaliyoko upande wa kusini watasafiri; 6watapiga sauti ya kugutusha kwa ajili ya safari zao. 7#Yoe 2:1Lakini mkutano utakapokutanishwa pamoja mtapiga, lakini hamtapiga sauti ya kugutusha. 8#Hes 31:6; Yos 6:4; 1 Nya 16:6; 2 Nya 13:12Wana wa Haruni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta; nazo zitakuwa kwenu ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote. 9#Amu 2:18; 3:27; 1 Sam 10:18; Zab 106:42; Mwa 8:1; 1 Fal 8:44; Zab 106:4Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu. 10#Law 23:24; 1 Nya 15:24; 2 Nya 7:6; Ezr 3:10; Neh 12:35; Zab 81:3; Kut 28:29; 30:16; Yos 4:7; 1 Kor 11:24-26Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Kuondoka toka Sinai
11 # Hes 9:17 Ikawa mwaka wa pili, mwezi wa pili, siku ya ishirini ya mwezi, hilo wingu liliinuka kutoka pale juu ya maskani ya ushahidi. 12#Kut 40:36; Hes 1:1; Kut 19:1; Hes 12:16; 13:3,26; Mwa 21:21; Kum 1:1; 32:2; 1 Sam 25:1; Hab 3:3Wana wa Israeli wakasafiri kwenda mbele, kwa safari zao kutoka jangwa la Sinai; na hilo wingu likakaa katika jangwa la Parani. 13#Hes 2:34Nao wakasafiri kwanza kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa. 14Mahali pa mbele ilisafiri beramu ya marago ya wana wa Yuda, kwa majeshi yao; na Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyekuwa juu ya jeshi lake. 15Na juu ya jeshi la kabila ya wana wa Isakari alikuwa Nethaneli mwana wa Suari. 16Na juu ya jeshi la kabila ya wana wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni. 17#Hes 1:51; 4:24,31Na maskani ilishushwa; na wana wa Gershoni, na wana wa Merari, walioichukua maskani, wakasafiri kwenda mbele. 18Kisha beramu ya marago ya Reubeni ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake alikuwa Elisuri mwana wa Shedeuri. 19Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Suri-shadai. 20Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli. 21Ndipo wakasafiri Wakohathi wenye kuvichukua vile vitu vitakatifu; na hao wengine wakaisimamisha maskani kabla hawajaja wao. 22Kisha beramu ya marago ya wana wa Efraimu ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Elishama mwana wa Amihudi. 23Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri. 24Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni. 25#Yos 6:9Kisha beramu ya marago ya wana wa Dani, ambayo yalikuwa ni nyuma ya marago yote, ikasafiri, kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Ahiezeri mwana wa Amishadai. 26Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani; 27Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani. 28#Zab 80:1; Wim 6:10Ndivyo zilivyokuwa safari zao wana wa Israeli kwa majeshi: yao; nao wakasafiri kwenda mbele.
29 # Kut 2:18; Mwa 12:7; Amu 1:16; 4:11; Mwa 32:12; Kut 6:7,8 Kisha Musa akamwambia Hobabu, mwana wa Reueli Mmidiani, mkwewe Musa, Sisi twasafiri kwenenda mahali ambapo BWANA amenena habari zake hivi, Nitawapa ninyi mahali hapo; uje pamoja nasi, nasi tutakufanyia mema; kwa kuwa BWANA ametamka mema juu ya Israeli. 30Naye akamwambia, Siendi mimi; ila nitairudia nchi yangu mwenyewe, na kwa jamaa zangu mwenyewe. 31#Ayu 29:15Naye akamwambia, Usituache, tafadhali; kwa kuwa wewe wajua jinsi tutakavyopanga nyikani, nawe utakuwa kwetu badala ya macho. 32Itakuwa, ukienda pamoja nasi, naam, itakuwa mema yo yote BWANA atakayotutendea sisi, tutakutendea wewe vivyo.
33 # Kut 3:2; Kum 1:33; Yer 31:2 Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa BWANA safari ya siku tatu; na sanduku la agano la BWANA likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika. 34#Kut 13:21; Neh 9:12,19; Zab 105:39Na wingu la BWANA lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini.
35 # Zab 68:1,2; Isa 51:9 Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema, Inuka, Ee BWANA, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao. 36#Zab 90:14,17; 132:8Tena hapo liliposimama, akasema, Ee BWANA, uwarudie maelfu kumi ya maelfu ya Israeli.

Currently Selected:

Hes 10: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy