Neh 5
5
Nehemia Akabiliana na Udhalimu
1 #
Isa 5:7; Yak 5:4; Law 25:35; Kum 15:7 Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu ya ndugu zao Wayahudi. 2#Mwa 41:57; Hag 1:6Maana, walikuwako watu waliosema, Sisi, na wana wetu na binti zetu, tu wengi; na tupate ngano, tule, tukaishi. 3Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa. 4Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu. 5#Mwa 37:27; Isa 58:7; Mdo 17:26; Kut 21:7; Mt 18:25Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu. 6#Kut 11:8; Neh 13:8; Mk 3:5; Efe 4:26Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. 7#Law 19:17; 1 Tim 5:20; Kut 22:25; Kum 23:19; Zab 15:5; Mit 27:5; Mt 18:17Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na mashehe, nikawaambia, Mnatoza watu riba, kila mtu ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kushindana nao. 8#Law 25:48Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lo lote. 9#Mwa 20:11; Law 25:36; Mdo 9:31; Mwa 13:7,8; 2 Sam 12:14; Rum 2:24; Tit 2:5; 1 Pet 2:12Tena nalisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu? 10Na mimi pia, na ndugu zangu, na watumishi wangu, twawakopesha fedha na ngano ili kupata faida? Tafadhali na tuliache jambo hili la riba. 11Naomba, warudishieni leo hivi mashamba yao, na mashamba yao ya mizabibu, na mashamba yao ya mizeituni, na nyumba zao, na lile fungu la mia la fedha, na la ngano, na la divai, na la mafuta, mnalowatoza. 12#Ezr 10:5; Yer 34:8,9Ndipo wakasema, Tutawarudishia, wala hatutataka kitu kwao; tutafanya hivyo, kama ulivyosema. Kisha nikawaita makuhani, nikawaapisha, ya kwamba watafanya kama ahadi hiyo. 13#Mt 10:14; Mdo 13:51; Zek 5:4; 2 Fal 23:3Tena nikakung’uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung’ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung’utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama ahadi hiyo.
Ukarimu wa Nehemia
14 #
Neh 13:6; 1 Kor 9:4 Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa liwali wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hata mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha liwali. 15#2 Kor 11:9; Mwa 42:18; Ayu 31:23; Zab 112:1; Mit 16:6; Mhu 12:13,14; Lk 18:2-4Lakini maliwali wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arobaini za fedha; tena watumwa wao nao wakatawala juu ya watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nalimcha Mungu. 16Naam, hata kazi ya ukuta huu tena nikaishika sana, wala hatukununua mashamba; na watumishi wangu wote wakakusanyika huko kazini. 17#2 Sam 9:7Pamoja na hayo wakawako mezani pangu, katika Wayahudi na mashehe, watu mia na hamsini, zaidi ya wale waliotujia kutoka kwa makafiri waliotuzunguka. 18#1 Fal 4:22Basi, maandalio yaliyoandaliwa kwa siku moja yalikuwa ng’ombe mmoja, na kondoo wazuri sita; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikukidai chakula cha liwali, kwa kuwa utumwa ulikuwa mzito juu ya watu hao. 19#Neh 13:22Unikumbukie, Ee Mungu wangu, kwa mema, yote niliyowafanyia watu hawa.
Currently Selected:
Neh 5: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.