YouVersion Logo
Search Icon

Law 19

19
Ibada na Maadili ya Utakatifu
1BWANA akanena na Musa, akamwambia, 2#Law 11:44-45; 20:7,26; 1 Pet 1:16; Kut 19:6; Efe 1:4; 1 The 4:7Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu. 3#Kut 20:8,12; 31:13; Kum 5:12,16; Mwa 2:2; Neh 9:14; 13:15-21; Isa 56:2; 58:13; Mk 2:27; Ebr 4:9Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 4#Law 26:1; Kut 20:3-5,23; 34:17; Kum 27:15; 1 Kor 10:14Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 5Nanyi hapo mtakapomchinjia BWANA sadaka ya amani mtaisongeza ili kwamba mpate kukubaliwa. 6Italiwa siku iyo hiyo mliyoichinja, na siku ya pili yake; na kama kitu cho chote katika sadaka hiyo kilisalia hata siku ya tatu kitachomwa moto. 7Kwamba sadaka hiyo yaliwa hata kidogo siku ya tatu ni machukizo; haitakubaliwa; 8lakini kila mtu atakayekula atauchukua uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha BWANA; na nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
9 # Law 23:22; Kum 15:1-18; 24:19-22; Kut 23:11; Rut 2:15 Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako; 10#Zab 41:1; 140:12; Mit 14:31; 22:16; Mhu 5:8; Isa 3:12-15; Yak 2:1-9wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako, wala usiyaokote matunda ya mizabibu yako yaliyopukutika; uyaache kwa ajili ya maskini na mgeni; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 11#Kut 20:15,16; Kum 5:19,20; 1 Fal 13:18; Yer 9:3-5; Mdo 5:3,4; Efe 4:25Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo. 12#Kut 20:7; Kum 5:11; Mt 5:33Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi BWANA. 13#Kum 24:14-15; Mal 3:5; Yak 5:4Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi. 14#Kum 27:18; Rum 14:13; 1 Pet 2:17Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA. 15#Kut 23:6-8; Kum 16:19; Zab 82:2; Mit 24:23; Yak 2:9Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki. 16#1 Fal 21:13; Mt 26:60Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA. 17#Mt 18:15; Mwa 27:41; 1 Yoh 2:9,11; 3:15; Lk 17:3Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. 18#Mt 5:43,44; 19:19; 22:39; Mk 12:31; Lk 10:27; Rum 13:9; 12:17; Gal 5:4; Yak 2:8Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA. 19#Kum 22:9-11Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. 20Tena mtu ye yote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mume, wala hakukombolewa kwa lo lote, wala hakupewa uhuru; wataadhibiwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru. 21Na huyo mume ataleta sadaka yake ya hatia aitoe kwa BWANA, hata mlangoni pa hema ya kukutania; kondoo mume kwa hiyo sadaka ya hatia. 22Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia mbele za BWANA, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya. 23Nanyi hapo mtakapoingia nchi ile, mkiwa mmepanda miti ya namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu matunda yake kama ni kutotahiriwa; muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu kama kutotahiriwa; matunda yake hayataliwa. 24#Kum 12:17,18Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni matakatifu, kwa ajili ya kumpa BWANA shukrani. 25Na katika mwaka wa tano mtakula katika matunda yake, ili ipate kuwapa maongeo yake; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 26#Mwa 9:4; Law 7:26-27; 17:10-14; Kum 12:16,23; 15:23; 18:10; 2 Fal 17:17Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. 27#Law 21:5; Kum 14:1; Yer 9:26Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu. 28#Kum 14:1Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA. 29#Kum 23:17Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu.
30 # Law 26:2; Mhu 5:1 Zishikeni Sabato zangu, mpaheshimu patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA. 31#Kum 18:11; 1 Sam 28:3; 2 Fal 23:4; Isa 8:19Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 32#1 Fal 2:19; Mit 20:29; 23:22; 1 Tim 5:1Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA. 33#Kut 22:21; Kum 24:17-18; 27:19Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu. 34#Kut 12:48; Kum 10:19Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 35#Kum 25:13-16; Mit 20:10; Eze 45:10Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. 36#Kum 25:13,15; Mit 20:10Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. 37#Kum 6:25; 5:1; Law 18:4,5Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA.

Currently Selected:

Law 19: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in