Omb 1
1
Mji Uliohamwa
1 #
Isa 47:7; Omb 1:9; Ezr 4:20 Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa,
Huo uliokuwa umejaa watu!
Jinsi alivyokuwa kama mjane,
Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa!
Binti mfalme kati ya majimbo,
Jinsi alivyoshikwa shokoa!
2 #
Yer 13:17; Omb 1:16; Ayu 7:3; Zab 6:6; Yer 4:30 Hulia sana wakati wa usiku,
Na machozi yake yapo mashavuni;
Miongoni mwa wote waliompenda
Hakuna hata mmoja amfarijiye;
Rafiki zake wote wamemtenda hila,
Wamekuwa adui zake.
3 #
Law 26:14,32,33; Kum 28:64 Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa,
Na kwa sababu ya utumwa mkuu;
Anakaa kati ya makafiri,
Haoni raha iwayo yote;
Wote waliomfuata wamempata
Katika dhiki yake.
4Njia za Sayuni zaomboleza,
Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu;
Malango yake yote yamekuwa ukiwa,
Makuhani wake hupiga kite;
Wanawali wake wanahuzunika;
Na yeye mwenyewe huona uchungu.
5 #
Yer 30:14; Omb 3:39 Watesi wake wamekuwa kichwa,
Adui zake hufanikiwa;
Kwa kuwa BWANA amemtesa
Kwa sababu ya wingi wa makosa yake;
Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka
Mbele yake huyo mtesi.
6Naye huyo binti Sayuni
Enzi yake yote imemwacha;
Wakuu wake wamekuwa kama ayala
Wasioona malisho;
Nao wamekwenda zao hawana nguvu
Mbele yake anayewafuatia.
7 #
Mik 4:11
Siku za mateso na misiba yake,
Yerusalemu huyakumbuka matamaniko yake yote
Yaliyokuwa tangu siku za kale;
Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi,
Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia;
Hao watesi wake walimwona,
Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
8 #
Yer 13:22
Yerusalemu amefanya dhambi sana;
Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu;
Wote waliomheshimu wanamdharau,
Kwa sababu wameuona uchi wake;
Naam, yeye anaugua,
Na kujigeuza aende nyuma.
9 #
Kum 32:29
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake;
Hakukumbuka mwisho wake;
Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu;
Yeye hana mtu wa kumfariji;
Tazama, BWANA, teso langu;
Maana huyo adui amejitukuza.
10 #
Kum 23:3; Neh 13:1 Huyo mtesi amenyosha mkono wake
Juu ya matamaniko yake yote;
Maana ameona ya kuwa makafiri wameingia
Ndani ya patakatifu pake;
Ambao kwa habari zao wewe uliamuru
Wasiingie katika kusanyiko lako.
11 #
Yer 38:9
Watu wake wote hupiga kite,
Wanatafuta chakula;
Wameyatoa matamaniko yao wapate chakula
Cha kuihuisha nafsi;
Ee BWANA, tazama, uangalie;
Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.
12 #
Dan 9:12; Mt 24:21; Lk 21:22 Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia,
Angalieni, mtazame
Kama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu,
Niliyotendwa mimi,
Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo
Siku ya hasira yake iwakayo.
13 #
Ayu 18:8; Zab 66:11; Eze 12:13; Hos 7:12 Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu,
Nao umeishinda;
Ametandika wavu aninase miguu,
Amenirudisha nyuma;
Amenifanya kuwa mtu wa pekee,
Na mgonjwa mchana kutwa.
14 #
Kum 28:48; Mit 5:22; Isa 14:25; Mt 11:29,30 Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake;
Hayo yameshikamana;
Yamepanda juu shingoni mwangu;
Amezikomesha nguvu zangu;
15 #
Isa 63:3; Ufu 14:19 Bwana amenitia mikononi mwao,
Ambao siwezi kupingamana nao.
Bwana amewafanya mashujaa wangu wote
Kuwa si kitu kati yangu;
Ameita mkutano mkuu kinyume changu
Ili kuwaponda vijana wangu;
Bwana amemkanyaga kama shinikizoni
Huyo bikira binti Yuda.
16Mimi ninayalilia mambo hayo;
Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji;
Kwa kuwa mfariji yu mbali nami,
Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi;
Watoto wangu wameachwa peke yao,
Kwa sababu huyo adui ameshinda.
17Sayuni huinyosha mikono yake;
Hakuna hata mmoja wa kumfariji;
BWANA ametoa amri juu ya Yakobo,
Kwamba wamzungukao wawe watesi wake;
Yerusalemu amekuwa kati yao
Kama kitu kichafu.
18 #
Neh 9:33; Dan 9:7; 1 Sam 12:14 BWANA ndiye mwenye haki;
Maana nimeiasi amri yake;
Sikieni, nawasihi, enyi watu wote,
Mkayatazame majonzi yangu;
Wasichana wangu na wavulana wangu
Wamechukuliwa mateka.
19Naliwaita hao walionipenda
Lakini walinidanganya;
Makuhani wangu na wazee wangu
Walifariki mjini;
Hapo walipokuwa wakitafuta chakula
ili kuzihuisha nafsi zao.
20 #
Isa 16:11; Yer 4:19; Hos 11:8; Kum 32:25 Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki;
Mtima wangu umetaabika;
Moyo wangu umegeuka ndani yangu;
Maana nimeasi vibaya sana;
Huko nje upanga hufisha watu;
Nyumbani mna kama mauti.
21 #
Yer 46:1
Wamesikia kwamba napiga kite;
Hakuna hata mmoja wa kunifariji;
Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata;
Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo;
Utaileta siku ile uliyoitangaza,
Nao watakuwa kama mimi.
22Huo uovu wao wote
Na uje mbele zako wewe;
Ukawatende wao kama ulivyonitenda mimi
Kwa dhambi zangu zote;
Kwa maana mauguzi yangu ni mengi sana,
Na moyo wangu umezimia.
Currently Selected:
Omb 1: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.