YouVersion Logo
Search Icon

Amu 5

5
Wimbo wa Debora
1Ndipo Debora, na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile, wakisema;
2Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli,
Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao,
Mhimidini BWANA.
3Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu;
Mimi, naam mimi, nitamwimbia BWANA;
Nitamhimidi BWANA, Mungu wa Israeli.
4 # Kum 33:2; Zab 68:7,8; Hab 3:3-6; Isa 64:3 BWANA, ulipotoka katika Seiri,
Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu,
Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondoza maji,
Naam, mawingu yakadondoza maji.
5 # Kut 19:18; Kum 4:11 Milima ikayeyuka mbele za uso wa BWANA,
Naam hata Sinai ule mbele za uso wa BWANA, Mungu wa Israeli.
6 # Amu 3:31; Law 26:22; Isa 33:8; Omb 1:4; 4:18 Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi,
Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu;
Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando.
7 # Amu 4:4-6; Isa 49:23 Maliwali walikoma katika Israeli, walikoma,
Hata mimi Debora nilipoinuka,
Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.
8 # Kum 32:16; Amu 2:12; 1 Sam 13:19,22; Amu 4:3 Walichagua miungu mipya,
Ndipo kulikuwa na vita malangoni;
Je! Ilionekana ngao au mkuki
Katika watu elfu arobaini wa Israeli?
9Moyo wangu unawaelekea maliwali wa Israeli,
Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu;
Mhimidini BWANA.
10 # Amu 12:14 Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe,
Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani,
Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.
11Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji,
Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA;
Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli.
Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.
12Amka, amka, Debora;
Amka, amka, imba wimbo.
Inuka, Baraka, wachukue mateka wao
Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.
13Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu;
BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.
14 # Amu 3:27; 4:5,6; Hes 32:39; Mwa 49:21 Kutoka Efraimu walitelemka wao ambao shina lao ni katika Amaleki,
Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako.
Kutoka Makiri walishuka maliwali,
Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.
15Na wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora.
Kama alivyokuwa Isakari, ndivyo alivyokuwa Baraka.
Waliingia bondeni kwa kasi miguuni pake.
Kwenye vijito vya Reubeni
Palikuwa na makusudi makuu mioyoni.
16 # Hes 32:1 Mbona ulikaa katika mazizi ya kondoo,
Kusikiliza filimbi zipigwazo ili kuita makundi?
Kwenye vijito vya Reubeni
Palikuwa na makusudi makuu mioyoni.
17 # Yos 13:25; 19:29 Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani,
Na Dani, mbona alikaa katika merikebu?
Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari,
Alikaa katika hori zake.
18 # Amu 4:10 Zabuloni ndio watu waliohatirisha roho zao hata kufa;
Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.
19 # Amu 4:16; Zab 44:12 Wafalme walikuja wakafanya vita,
Ndipo wafalme wa Kanaani walifanya vita.
Katika Taanaki, karibu na maji ya Megido;
Hawakupata faida yo yote ya fedha.
20 # Yos 10:11; Amu 4:15 Walipigana kutoka mbinguni,
Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.
21 # Amu 4:7 Mto ule wa Kishoni uliwachukua,
Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.
Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu.
22Ndipo kwato za farasi zilikanyaga-kanyaga
Kwa sababu ya kupara-para,
Kupara-para kwao wenye nguvu.
23 # Amu 21:9; Neh 3:5; 1 Sam 17:47 Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA,
Walaanini kwa uchungu wenyeji wake;
Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA,
Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.
24 # Mit 31:31; Lk 1:28 Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote;
Mkewe Heberi, Mkeni,
Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani.
25Aliomba maji, naye akampa maziwa.
Akamletea siagi katika sahani ya heshima.
26Akanyosha mkono wake akashika kigingi,
Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi;
Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake.
Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake.
27Miguuni pake aliinama, akaanguka, akalala.
Miguuni pake aliinama, akaanguka.
Hapo alipoinama, ndipo alipoanguka amekufa.
28Alichungulia dirishani, akalia,
Mama yake Sisera alilia dirishani;
Mbona gari lake linakawia kufika?
Mbona gurudumu za gari lake zinakawia?
29Mabibi yake wenye akili wakamjibu,
Naam, alijipa nafsi yake jawabu.
30 # Kut 15:9 Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya,
Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu?
Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbali mbali,
Nyara za mavazi ya rangi mbali mbali ya darizi;
Ya rangi mbali mbali ya darizi, pande zote mbili,
Juu ya shingo za hao mateka.
31 # Zab 48:4,5; 58:11; Ufu 6:10; 18:20; 2 Sam 23:4; Zab 37:6; Mt 13:43; Zab 19:5 Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA.
Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arobaini.

Currently Selected:

Amu 5: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy