YouVersion Logo
Search Icon

Isa 62

62
Uthibitisho wa Wokovu wa Sayuni
1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 2#Isa 65:15; Ufu 3:12Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA. 3#Zek 9:16Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4#Hos 1:10; 1 Pet 2:10Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba;#62:4 Hefsiba maana yake ni Namfurahia. na nchi yako Beula;#62:4Beula maana yake ni Ameolewa. kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 5Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
6 # Wim 3:3; Isa 52:8; Eze 3:17; Ebr 13:17 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya; 7#Isa 61:11; Sef 3:20wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani. 8#Kum 28:31; Yer 5:17BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. 9#Kum 12:12Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
10Piteni, piteni, katika malango;
Itengenezeni njia ya watu;
Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;
Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.
11 # Zek 9:9; Mt 21:5; Yn 12:15; Isa 40:10; 49:4; Ufu 22:12 Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,
Mwambieni binti Sayuni,
Tazama, wokovu wako unakuja;
Tazama, thawabu yake i pamoja naye,
Na malipo yake yako mbele zake.
12Nao watawaita, Watu watakatifu,
Waliokombolewa na BWANA;
Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,
Mji usioachwa.

Currently Selected:

Isa 62: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in