Isa 52
52
Sayuni Ishangilie
1 #
Nah 1:15; Isa 26:2; Ufu 21:2,27 Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni;
Jivike mavazi yako mazuri,
Ee Yerusalemu, mji mtakatifu;
Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako
Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.
2 #
Zek 2:7
Jikung’ute mavumbi; uondoke,
Uketi, Ee Yerusalemu;
Jifungulie vifungo vya shingo yako,
Ee binti Sayuni uliyefungwa.
3 #
Zab 44:12; 1 Pet 1:18 Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha. 4Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu. 5#Rum 2:24Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa. 6Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.
7 #
Nah 1:15; Rum 10:15; Efe 6:15 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima
Miguu yake aletaye habari njema,
Yeye aitangazaye amani,
Aletaye habari njema ya mambo mema,
Yeye autangazaye wokovu,
Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
8 #
Sef 3:9
Sauti ya walinzi wako!
Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja;
Maana wataona jicho kwa jicho,
Jinsi BWANA arejeavyo Sayuni.
9Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja,
Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa;
Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,
Ameukomboa Yerusalemu.
10 #
Lk 3:6
BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu
Machoni pa mataifa yote;
Na ncha zote za dunia
Zitauona wokovu wa Mungu wetu.
11 #
Yer 50:8; Ufu 18:4; 2 Kor 6:17 Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA. 12#Kut 12:33; 14:19; Mik 2:13; Hes 10:25Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.
Mtumishi Atesekaye
13 #
Isa 42:1; Flp 2:9 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. 14#Zab 22:6; Isa 53:3Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), 15#Eze 36:25; Mdo 2:33; Ebr 9:13; Efe 3:5; Rum 15:21ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.
Currently Selected:
Isa 52: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.