YouVersion Logo
Search Icon

Isa 32

32
Ufalme wenye Haki Watabiriwa
1 # 2 Nya 31:20; Zab 7:1,2; Yer 23:5; Zek 9:9; Ebr 1:8,9; Ufu 19:11 Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu. 2Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu. 3#Isa 29:18Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza. 4Tena moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa. 5Mpumbavu hataitwa tena mwungwana, wala ayari hatasemwa kwamba ni karimu. 6Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu. 7Tena vyombo vyake ayari ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki. 8Bali mwungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.
Wanawake Wasiojali Waonywa juu ya Maafa
9 # Amo 6:1 Inukeni, enyi wanawake wenye raha, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiokuwa na uangalifu, tegeni masikio yenu msikie matamko yangu. 10Maana mtataabishwa siku kadha wa kadha zaidi ya mwaka, enyi wanawake mliojikinai; kwa sababu mavuno ya mizabibu yatakoma, wakati wa kuvuna vitu vya mashamba hautakuja. 11Tetemekeni, enyi wanawake wenye raha; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu; jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, jivikeni viuno nguo za magunia. 12Watajipiga vifua kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mzabibu uliozaa sana. 13#Hos 9:6Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe; 14maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda-mwitu, malisho ya makundi ya kondoo; 15#Zab 104:30hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.
Amani ya Utawala wa Mungu
16 # Zek 8:3 Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana. 17#Zab 72:2,3; Mik 4:4,5; Lk 2:14Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. 18Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. 19#Zek 11:2Lakini mvua ya mawe itakunya, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika. 20#Isa 30:24Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng’ombe na punda waende ko kote.

Currently Selected:

Isa 32: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy