YouVersion Logo
Search Icon

Isa 27

27
Ukombozi wa Israeli
1 # Eze 29:3; Ayu 41:1; Zab 74:14; 104:26 Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. 2Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
3Mimi, BWANA, nalilinda,
Nitalitia maji kila dakika,
Asije mtu akaliharibu;
Usiku na mchana nitalilinda.
4 # 2 Sam 23:6 Hasira sinayo ndani yangu;
Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu,
Ningepanga vita juu yake,
Ningeiteketeza yote pamoja.
5 # Ayu 22:21; Isa 53:4,5; Efe 2:12-14 Au azishike nguvu zangu,
Afanye amani nami;
Naam, afanye amani nami.
6 # Isa 37:31; Hos 14:5,6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi;
Israeli atatoa maua na kuchipuka;
Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
7Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye? 8#Ayu 23:6; Zab 6:1; Yer 10:24; 1 Kor 10:13Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki. 9Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena. 10#Isa 17:2Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake. 11#Kum 32:18,28; Zab 28:5; Isa 1:3; 44:2,21,24; Yer 4:22; 2 The 1:8Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
12Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
13 # Isa 2:11; Hes 10:2; Zab 81:3; Hos 8:1; Mt 24:31; Ufu 11:15 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

Currently Selected:

Isa 27: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in