YouVersion Logo
Search Icon

Hos 12

12
1 # 2 Fal 17:4; Isa 30:6 Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.
Uasi wa Muda Mrefu
2BWANA naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.
3 # Mwa 25:26 # Mwa 32:24-26 Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;
Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;
4 # Mwa 28:10-22 Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika
Akashinda; alilia, na kumsihi;
Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
5Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;
BWANA ndilo kumbukumbu lake.
6Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
7Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu. 8Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi. 9#Law 23:42-43Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi. 10Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano. 11#Amo 4:4Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.
12 # Mwa 29:1-20 Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,
Na Israeli alitumika apate mke;
Ili apate mke alichunga kondoo.
13 # Kut 12:50-51 Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,
Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.
14 # Kum 28:37; Dan 11:18 Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.

Currently Selected:

Hos 12: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in