Hos 1
1
1 #
2 Pet 1:21; 2 Fal 14:23-29; 15:1-7,32-38; 16:1-20; 18:1—20:21; 2 Nya 26:1—27:8; 28:1—32:33 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Hosea, mwana wa Beeri, siku za Uzia, na Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli.
Familia ya Hosea
2 #
Kum 31:16; Amu 2:17; Zab 73:27 Hapo kwanza BWANA aliponena kwa kinywa cha Hosea, BWANA alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha BWANA. 3Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Diblaimu; naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamume. 4#2 Fal 10:11BWANA akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli. 5Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli. 6Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama#1:6Lo-ruhama maana yake ni Asiyehurumiwa.; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yo yote. 7Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi. 8Basi, akiisha kumwachisha Lo-ruhama, akachukua mimba, akazaa mtoto mwanamume. 9BWANA akasema, Mwite jina lake Lo-ami#1:9Lo-ami maana yake ni Si watu wangu.; kwa maana ninyi si watu wangu, wala mimi sitakuwa Mungu wenu.
Matengenezo ya Israeli
10 #
Mwa 26:4; Kut 32:13; Hes 23:10; Kum 1:10; 1 Fal 3:8; 1 Nya 27:23; Yn 1:12; Rum 9:26 Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai. 11Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.
Currently Selected:
Hos 1: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.