YouVersion Logo
Search Icon

Ebr 10

10
Kafara ya Kristo Inatosha
1 # Ebr 8:5; 7:19 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. 2Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? 3#Law 16:21Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. 4Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. 5#Zab 40:6-8Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,
Dhabihu na toleo hukutaka,
Lakini mwili uliniwekea tayari;
6Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;
7Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa)
Niyafanye mapenzi yako, Mungu.
8Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), 9ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. 10#Ebr 9:12,28Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. 11#Kut 29:38Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. 12#Zab 110:1Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; 13tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. 15Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema,
16 # Yer 31:33; Ebr 8:10 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana,
Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,
Na katika nia zao nitaziandika;
ndipo anenapo,
17 # Yer 31:34; Ebr 8:12 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
18Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
Wito wa kuwa Wavumilivu
19 # Mt 27:51 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20#Ebr 9:8njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 21#Zek 6:11; Hes 12:7na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22#Law 8:30; Eze 36:25; Efe 5:26na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi. 23#Ebr 4:14Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu; 24#Ebr 13:1tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; 25#Ebr 3:13wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
26 # Ebr 6:4-8; 1 Tim 2:4 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27#Isa 26:11bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. 28#Kum 17:6; 19:15; Hes 15:30; 35:30Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29#Kut 24:8; Ebr 2:3Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? 30#Kum 32:35-36; Zab 135:14; Rum 12:19Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. 31#Ebr 12:29Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.
32 # Ebr 6:4 Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; 33#1 Kor 4:9pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. 34#Mt 6:20; 19:21,29Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. 35#Ebr 11:6Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. 36#Ebr 6:12; Lk 21:19Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.
37 # Hab 2:3-4; Isa 26:20; Lk 21:28; Yak 5:8 Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana,
Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
38 # Rum 1:17; Gal 3:11 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
39Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.

Currently Selected:

Ebr 10: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy