YouVersion Logo
Search Icon

Mwa 49

49
Wosia wa Yakobo kwa Wanawe
1 # Kum 4:30; 33:1; Amo 3:7; Hes 24:14 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2 # Zab 34:11 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,
Msikilizeni Israeli, baba yenu.
3 # Kum 21:17 Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,
Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu.
Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.
4 # Kum 27:20; 1 Nya 5:1 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu,
Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako,
Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.
5 # Mit 18:9; Mwa 34:25 Simeoni na Lawi ni ndugu;
Panga zao ni silaha za jeuri.
6 # Mit 1:15; Zab 26:9 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao,
Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao,
Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu,
Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe;
7 # Yos 21:1; 1 Nya 4:24 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali,
Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.
Nitawagawa katika Yakobo,
Nitawatawanya katika Israeli.
8Yuda, ndugu zako watakusifu,
Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako.
Wana wa baba yako watakuinamia.
9 # Hes 24:9 Yuda ni mwana-simba,
Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda;
Aliinama akajilaza kama simba,
Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?
10 # Hes 24:17; Zab 60:7; 1 Nya 5:2; Isa 11:1; Eze 21:27; Dan 9:25; Mt 21:9; Lk 1:32; Isa 2:2; 11:10; 60:1-5; Hag 2:7; Lk 2:30; 2 Fal 18:32 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,
Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,
Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,
Ambaye mataifa watamtii.
11Atafunga punda wake katika mzabibu,
Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri.
Amefua nguo zake kwa mvinyo,
Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
12Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo,
Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
13 # Kum 33:18 Zabuloni atakaa pwani ya bahari,
Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu,
Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
14Isakari ni punda hodari,
Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;
15Akaona mahali pa raha, kuwa pema,
Na nchi, ya kuwa ni nzuri,
Akainama bega lake lichukue mizigo,
Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
16 # Amu 13:2; 15:20 Dani atahukumu watu wake,
Kama moja ya makabila ya Israeli;
17 # Amu 18:27 Dani atakuwa nyoka barabarani,
Bafe katika njia,
Aumaye visigino vya farasi,
Hata apandaye ataanguka chali.
18 # Zab 25:3,5; 62:5; Isa 25:9; 40:31; Rum 2:7; 1 Kor 1:7; Flp 3:20; Tit 2:13 Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.
19 # Kum 33:20 Gadi, jeshi litamsonga,
Lakini atawasonga wao mpaka visigino.
20Asheri, chakula chake kitakuwa kinono,
Naye atatoa tunu za kifalme.
21Naftali ni ayala aliyefunguliwa;
Anatoa maneno mazuri.
22Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa,
Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi,
Matwi yake yametanda ukutani.
23 # Mwa 37:24 Wapiga mishale walimtenda machungu,
Wakamtupia, wakamwudhi,
24 # Ayu 29:20; Zab 132:2,5; 80:1; Isa 28:16 Lakini upinde wake ukakaa imara,
Mikono yake ikapata nguvu,
Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo;
Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli,
25 # Kum 33:13 Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia;
Kwa mibaraka ya mbinguni juu.
Mibaraka ya vilindi vilivyo chini,
Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.
26Mibaraka ya baba yako
Imepita mibaraka ya milima ya kale,
Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele;
Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu,
Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.
27 # Amu 20:21,25; Hes 23:24; Est 8:11; Eze 39:10; Zek 14:1,7 Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua
Asubuhi atakula mawindo,
Na jioni atagawanya mateka.
28Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki.
Kufa kwa Yakobo na Kuzikwa kwake
29 # Mwa 15:15; 25:8; 2 Sam 19:37; Mwa 47:30; 50:13 Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; 30#Mwa 23:16katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. 31#Mwa 23:19; 25:9; 35:29Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; 32shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi. 33Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.

Currently Selected:

Mwa 49: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy