YouVersion Logo
Search Icon

Mwa 12

12
Abramu Aitwa na Mungu
1 # Mdo 7:2-3; Ebr 11:8; Mwa 15:7 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2#Mwa 17:6; 18:18; 46:3; Hes 23:10; Kum 26:5; 1 Fal 3:8nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3#Gal 3:8; Mwa 24:35; 27:29; Kut 23:22; Hes 24:9; Mwa 22:18; 26:4; 28:14; Zab 72:17; Mdo 3:25nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. 4Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani. 5#Mwa 11:31; Ebr 11:8Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani. 6#Yn 4:5; Kum 11:30; Amu 7:1Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. 7#Mdo 7:5; Gal 3:16; Mwa 17:1; Kum 34:4; Zab 105:9-12; Mwa 13:4BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea. 8Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. 9#Mwa 13:3Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini.
Abramu na Sarai nchini Misri
10 # Mwa 26:1; Zab 105:13; Mwa 43:1 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. 11#Mwa 26:7Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; 12#Mwa 20:11basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. 13#Mwa 20:2; 26:7; Zab 25:21; Efe 4:25Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako. 14Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana. 15#Est 2:16Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao. 16Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng’ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia. 17#Mwa 20:18; 1 Nya 16:21; Zab 105:14; Ebr 13:4Lakini BWANA akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu. 18#Mwa 20:9; 26:10; Mit 21:1Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema, N’nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo? 19Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako. 20Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho.

Currently Selected:

Mwa 12: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in