YouVersion Logo
Search Icon

Gal 4

4
1Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; 2bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba. 3#Gal 3:23; 5:1; Kol 2:20Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia. 4#Efe 1:10Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5#Rum 8:15-17#Gal 3:13,26kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. 6#Rum 8:15Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. 7#Gal 3:29; Rum 8:16,17Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Paulo Awashutumu Wagalatia
8Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu. 9Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? 10#Rum 14:5; Kol 2:16Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka. 11#2 Yoh 1:8Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha bure kwa ajili yenu.
12 # 2 Kor 2:5 Ndugu zangu, nawasihi, iweni kama mimi, maana mimi ni kama ninyi. Hamkunidhulumu kwa lo lote. 13#Mdo 16:6; 1 Kor 2:3Lakini mwajua ya kuwa naliwahubiri Injili mara ya kwanza kwa sababu ya udhaifu wa mwili; 14#Mdo 14:11,12na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu. 15Ku wapi, basi, kule kujiita heri? Maana nawashuhudu kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling’oa macho yenu, mkanipa mimi. 16#Amo 5:10Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli? 17#Gal 1:7Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa njia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku. 18Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu. 19#1 Kor 4:15Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu; 20laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu.
Mfano wa Hajiri na Sara
21 # Gal 3:23 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22#Mwa 16:15; 21:2,9Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23#Rum 9:7-9; Mwa 17:16Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24#Gal 5:1; Rum 8:15Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. 26#Ebr 12:22Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27#Isa 54:1Kwa maana imeandikwa,
Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa;
Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu;
Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi
Kuliko wa huyo aliye na mume.
28Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29#Mwa 21:9Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30#Mwa 21:10,12; Yn 8:35Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31#Gal 3:29Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.

Currently Selected:

Gal 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy