Kut 23
23
Haki kwa Wote
1 #
Kut 20:16; Law 19:11-12; Kum 5:20; Mit 10:18; 1 Fal 21:10; Mit 19:5; Mdo 6:11 Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. 2#1 Fal 19:10; Ayu 31:34; Lk 23:23; Zab 72:2Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; 3#Law 19:15wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. 4#Kum 22:1-4; Mit 25:21; 1 The 5:15Ukimwona ng’ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. 5Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
6 #
Law 19:15; Kum 16:19; Ayu 31:13 Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. 7#Efe 4:25; Rum 1:18Jitenge mbali na neno uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu. 8#Mit 17:8Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki. 9#Zab 94:6; Kut 22:21; Law 19:33-34; Kum 24:17-18; 27:19Usimwonee mgeni; maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
Sheria kuhusu Mwaka wa Saba na Sabato
10 #
Law 25:1-7
Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; 11lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni. 12#Lk 13:14; Kut 20:9-11; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Kum 5:13-14Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng’ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika. 13#Hos 2:17Yaangalieni hayo yote niliyowaambia; wala msitaje kabisa majina ya miungu mingine, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako.
Sikukuu za Kila Mwaka
14 #
Kum 16:16
Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu. 15#Kut 12:14-20; Law 23:6-8; Hes 28:17-25Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu; 16#Law 23:15-21,39-43; Hes 28:26-31tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. 17Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU.
18Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. 19#Kut 34:26; Kum 14:21; 26:2; Neh 10:35; Mit 3:9Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Kuahidiwa Ushindi juu ya Kanaani
20Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. 21#Efe 4:30; Yos 24:19; 1 Yoh 5:16; Isa 9:6; Yer 23:6; Yn 10:38Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 22#Mwa 12:3Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 23#Yos 24:8Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. 24#Kut 20:5Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. 25#Kum 10:12; Yos 22:5; 1 Sam 2:20; Mt 4:10; Kum 7:15; 28:5Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26#Ayu 21:10; Mwa 25:8Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. 27#Mwa 35:5; Kum 2:25; Yos 2:9,11; 1 Sam 14:15Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. 28#Kum 7:20Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. 29#Kum 7:22Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. 30Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi. 31#1 Fal 4:21; Yos 21:44Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako. 32Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao. 33#Kut 34:12,15; Kum 7:2; 12:30; Yos 23:13; Amu 2:3; 1 Sam 18:21; Zab 106:36,37Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako.
Currently Selected:
Kut 23: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.