Kum 29
29
Agano Kufanywa Upya katika Moabu
1Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.
2Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote BWANA aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote; 3#Kum 4:34; 7:19yale majaribu makuu yaliyoyaona macho yako; hizo ishara, na ile miujiza mikuu; 4#Zab 13:3; 19:8; Isa 6:9; 63:17; Eze 12:2; Mt 13:14; Yn 8:43; Mdo 28:26; Rum 11:8; Efe 1:18; 4:17-19; 2 The 2:11lakini BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi. 5#Kum 1:3; 8:2Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako. 6#Kut 16:12; Neh 9:15; Zab 78:24Hamkula mkate, wala hamkunywa divai, wala kileo; ili mpate kujua kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 7#Hes 21:21-35; Kum 2:32; 3:1Nanyi mlipokuja mahali hapa, walitutokea kupigana juu yetu Sihoni mfalme wa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, tukawapiga; 8#Hes 32:33tukaitwaa nchi yao, nayo tukawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase, iwe urithi. 9#Yos 1:7; 1 Fal 2:3; Zab 25:10; 103:17,18; Isa 56:1,2,4,7; Yer 1:5Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo.
10Leo mmesimama nyote mbele za BWANA, Mungu wenu; wakuu wenu, na kabila zenu, na wazee wenu, na maakida wenu, waume wote wa Israeli, 11#Yos 9:21vijana vyenu, na wake wenu, na mgeni wako aliye kati ya kituo chako, tokea mchanjaji wa kuni zako hata mtekaji wa maji yako; 12ili uingie katika agano la BWANA, Mungu wako, na kiapo chake, afanyacho nawe BWANA, Mungu wako, hivi leo; 13#Mwa 17:6,7apate kukuweka leo uwe taifa kwake naye apate kuwa Mungu kwako, kama alivyokuambia, na kama alivyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo. 14#Yer 31:31; Ebr 8:7,8Wala sifanyi na ninyi peke yenu agano hili na kiapo hiki; 15#Mdo 2:39; 1 Kor 7:14ila na yeye aliyesimama hapa nasi hivi leo mbele ya BWANA, Mungu wetu, na yeye naye asiyekuwapo pamoja nasi leo; 16(kwani mwajua mlivyoketi nchi ya Misri, na tulivyo kuja katikati ya mataifa hayo mliyopita katikati yao; 17nanyi mliona machukizo yao, na sanamu zao, miti na mawe, fedha na dhahabu, zilizokuwako kwao;) 18#Ebr 12:15asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache BWANA, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga; 19#Zab 14:1; Hes 15:39; Yer 7:24; Ayu 15:16; 34:7; Isa 30:1; 56:12; Efe 4:19ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu; 20#Eze 14:7; 23:25; Zab 74:1; 79:5BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu. 21#Mt 24:51BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika chuo hiki cha torati. 22Na kizazi cha baadaye, wanenu watakaoinuka baada yenu, na mgeni atakayekuja kutoka nchi ya mbali, watasema, watakapoyaona mapigo ya nchi ile, na magonjwa aliyoitia BWANA; 23#Mwa 19:24-25; Amu 9:45; Zab 107:34; Yer 17:6; Eze 47:11; Sef 2:9; Lk 14:34,35ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake; 24#1 Fal 9:8; Yer 22:8mataifa yote watasema, Mbona BWANA ameifanyia hivi nchi hii? Ni nini maana yake hari ya hasira hizi kubwa? 25Ndipo watakaposema watu, Ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri; 26wakaenda wakatumikia miungu mingine, wakaiabudu miungu wasiyoijua, asiyowapa yeye; 27#Zab 11:6; Dan 9:11ndipo ikawashwa hasira ya BWANA juu ya nchi hii, kwa kuleta juu yake laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki; 28#2 Nya 7:20; Ayu 11:6,7; Zab 52:5; Mit 2:22; 3:22BWANA akawang’oa katika nchi yao kwa hasira, na ghadhabu, na makamio makuu, akawatupa waende nchi nyingine, kama hivi leo. 29#Ayu 11:6,7; Mit 3:32; Yer 23:18; Amo 3:7; Mdo 1:7; Zab 19:7; Lk 16:29; Yn 5:39; Mdo 17:11; 2 Tim 3:16Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
Currently Selected:
Kum 29: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.