Kum 27
27
Mawe yenye Maandishi na Madhabahu katika Mlima
1Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza wale watu wakawaambia, Shikeni maagizo yote niwaagizayo leo. 2#Yos 4:1; 8:30-32Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo BWANA, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo, 3uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi BWANA, Mungu wa baba zako. 4#Kum 11:29; Yos 8:30Na iwe, mtakapokwisha vuka Yordani myasimamishe mawe haya, niwaagizayo hivi leo, katika mlima Ebali, nawe yatalize matalizo. 5#Kut 20:25; Yos 8:31Na huko umjengee madhabahu BWANA, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. 6Jenga hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee BWANA, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake; 7ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako. 8#Hab 2:2Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana.
9Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako. 10Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo.
11Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema, 12#Kum 11:29; Yos 8:33-35; Amu 9:7Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; 13na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali. 14#Kum 33:10; Yos 8:33; Neh 8:7,8; Dan 9:11; Mal 2:7-9Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu,
15 #
Kut 20:4; 34:17; Law 19:4; 26:1; Kum 4:15-18; 5:8; Isa 44:9; Hos 13:2; Hes 5:22; Yer 11:5; 1 Kor 14:16 Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
16 #
Kut 20:12; Kum 5:16; Law 19:3 Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
17 #
Kum 19:14; Mit 22:28 Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.
18 #
Law 19:14; Ayu 29:15; Mit 28:10; Mt 15:14; Ufu 2:14 Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.
19 #
Kut 22:21; 23:9; Law 19:33-34; Kum 10:18; 24:17-18; Mal 3:5 Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
20 #
Law 18:8; 20:11; Kum 22:30; 1 Kor 5:1 Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.
21 #
Kut 22:19; Law 18:23; 20:15 Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.
22 #
Law 18:9; 20:17; 2 Sam 13:1 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.
23 #
Law 18:17; 20:14 Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.
24 #
Law 24:17; Hes 35:31 Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.
25 #
Kut 23:7; Kum 10:17; 16:19; Zab 15:5; Eze 22:12 Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.
26 #
Gal 3:10; Zab 119:21; Yer 11:3 Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Currently Selected:
Kum 27: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.