YouVersion Logo
Search Icon

2 Nya 8

8
Mengine Aliyotenda Sulemani
1 # 1 Fal 9:10 Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani aliijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe; 2ndipo Sulemani akaijenga miji ile Hiramu aliyompa Sulemani, akawakalisha humo wana wa Israeli.
3 # Hes 13:21; 2 Sam 8:3 Naye Sulemani akaenda Hamath-zoba, akaushinda. 4#1 Fal 9:17Akaujenga Tadmori wa nyikani, na miji yote ya hazina, aliyoijenga katika Hamathi. 5Tena akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye boma, yenye kuta, na malango, na makomeo; 6#Yos 15:11na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 7#1 Fal 9:20; Mwa 10:15; 15:18; Kum 7:1Basi kwa habari ya watu wote waliosalia wa Wahiti, na wa Waamori, na wa Waperizi, na wa Wahivi, na wa Wayebusi, wasiokuwa wa Israeli; 8wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 9#Kut 19:5; Kum 23:19; Law 25:39; Gal 4:28,31Wala katika wana wa Israeli Sulemani hakuwafanya watumwa kazini mwake; lakini hao walikuwa watu wa vita, na wakuu wa majemadari wake, na maakida wa magari yake na wa wapanda farasi wake. 10#1 Fal 5:16; 9:23; 2 Nya 2:18Na hao walikuwa maakida wakuu wa Sulemani, watu mia mbili na hamsini, waliotawala juu ya watu. 11#1 Fal 3:1; 7:8; 9:24Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la BWANA.
12Ndipo Sulemani akamtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya BWANA, aliyoijenga mbele ya ukumbi, 13#Kut 29:38; Hes 28:3-26; 29:1; Kut 23:14; Kum 16:16; 1 Fal 9:25kadiri ilivyohitajiwa huduma ya kila siku, akitoa sawasawa na amri ya Musa, siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoamriwa, mara tatu kila mwaka, yaani, sikukuu ya mikate isiyochachwa, na sikukuu ya majuma, na sikukuu ya vibanda. 14#1 Nya 24:1; 2 Nya 5:11; 31:2; Lk 1:5,8; 1 Nya 25:1; 9:17; 26:1; 2 Sam 23:2Akaziamuru, sawasawa na agizo la Daudi babaye, zamu za makuhani za kutumika, nao Walawi kwa kadiri ya malinzi yao, ili kusifu, na kuhudumu mbele ya makuhani, kama ilivyohitajiwa kila siku; tena mabawabu kwa zamu zao za kila mlango; maana ndivyo alivyoamuru Daudi mtu wa Mungu. 15Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lo lote, wala kwa habari ya hazina. 16Basi ikatengenezwa kazi yote ya Sulemani hata siku ya kutiwa msingi wa nyumba ya BWANA, na hata ilipokwisha. Hivyo ikamalizika nyumba ya BWANA.
17 # 1 Fal 9:26; Kum 2:8; 2 Fal 14:22 Ndipo Sulemani akaenda Esion-geberi, na Elothi, pwani ya nchi ya Edomu. 18#1 Fal 9:27; 2 Nya 9:10,13; Mwa 10:29; Ayu 22:24; Isa 13:12Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wana-maji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.

Currently Selected:

2 Nya 8: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in