1 Tim 3
3
Sifa za Maaskofu
1 #
Mdo 20:28
Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu,#3:1Askofu maana yake ni, Mwangalizi. atamani kazi njema. 2#Tit 1:6-9Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; 3si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; 4#1 Sam 2:12mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; 5(yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) 6Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 7#1 Tim 5:10; 2 Kor 8:21; 1 Kor 5:12,13Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Sifa za Mashemasi
8 #
Flp 1:1; Mdo 6:3 Vivyo hivyo mashemasi#3:8Shemasi maana yake ni, Mtumishi wa Kanisa.8 na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; 9wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. 10Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. 11#Tit 2:3Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. 12Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. 13Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Siri ya Dini Yetu
14Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. 15#2 Tim 2:20; Efe 2:19-22Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 16#Yn 1:14; 16:10; Rum 1:4; Mk 16:19Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.
Mungu alidhihirishwa katika mwili,
Akajulika kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na malaika,
Akahubiriwa katika mataifa,
Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.
Currently Selected:
1 Tim 3: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.