YouVersion Logo
Search Icon

1 Sam 7

7
1 # 2 Sam 6:2-4; 1 Nya 13:5-7; 1 Sam 6:21; Zab 132:6 Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA.
2Ikawa, tangu siku hiyo ambayo sanduku lilikaa Kiriath-yearimu wakati ulikuwa mwingi; kwa maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Israeli wakamwombolezea BWANA.
Samweli awa Mwamuzi
3 # Kum 30:2; 1 Fal 8:48; Isa 55:7; Hos 6:1; Yoe 2:12; Mwa 35:2; Yos 24:14; Amu 2:13; 2 Nya 30:19; Mt 4:10; 15:8; Lk 4:8 Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti. 4Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia BWANA peke yake.
5 # Amu 10:17; 11:11; 1 Sam 10:17; 2 Fal 25:23 Samweli akasema, Wakusanyeni Israeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA. 6#2 Sam 14:14; Neh 9:1,2; Dan 9:3; Yoe 2:12; Law 26:40; Amu 10:10; 1 Fal 8:47; Ayu 33:27,28; Zab 106:6Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia BWANA dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa. 7Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. 8#Isa 37:4Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti. 9#Zab 99:6; Yer 15:1Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia. 10#Yos 10:10; Amu 4:15; 1 Sam 2:10; 2 Sam 22:14,15Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli. 11Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga, hata walipofika chini ya Beth-kari.
12 # 1 Sam 4:1 Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia. 13#Amu 13:1; 1 Sam 13:5Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli. 14Nayo miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa tena kwa Israeli, tokea Ekroni mpaka Gathi; na Waisraeli wakauokoa mpaka wake mikononi mwa Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Israeli na Waamori. 15#1 Sam 12:11; Amu 2:16Naye huyo Samweli akawaamua Israeli siku zote za maisha yake. 16Naye huenda mwaka kwa mwaka kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua Israeli mahali hapo pote. 17#Amu 21:4Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.

Currently Selected:

1 Sam 7: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in