YouVersion Logo
Search Icon

1 Fal UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kuna vitabu viwili vya Wafalme, cha Kwanza na cha Pili. Vitabu hivi vilikuwa kitabu kimoja katika Biblia ya zamani ya Kiebrania, kiliitwa “Wafalme”. Watafsiri wa toleo la lugha ya Kigiriki liitwalo “Septuaginta” walikigawanya katika sehemu mbili ambazo zimekuwa vitabu viwili vya Wafalme tulivyo navyo sasa. Jina Wafalme linatokana na masimulizi yaliyomo katika vitabu hivi.
Vitabu vya Wafalme vinasimulia yaliyotukia katika Israeli kwa muda wa takriban karne nne. Kuanzia mwanzoni mwa utawala wa mfalme Daudi hadi mwisho wa utawala wa kifalme katika Israeli. Mwandishi wa vitabu hivi hajulikani jina lake.
Masimulizi ya sehemu ya kwanza iitwayo Kitabu cha Kwanza cha Wafalme yanaanzia pale Kitabu cha Samweli kilipokomea. Wakati wa utawala wa Sulemani, Waisraeli walistawi sana, Hekalu lilijengwa wakawa na sifa ya uchaji Mungu, nguvu kisiasa, utajiri na heshima. Lakini kipindi hicho kilikuwa kifupi. Baada ya kifo cha Sulemani mambo yalivurugika. Ufalme uligawanyika ukawa falme mbili zilizopingana. Upande wa Kaskazini ukaitwa Ufalme wa Israeli na upande wa kusini ukaitwa Ufalme ya Yuda (12–14). Umoja kidini na kitaifa ulikwisha. Wafalme wengi hawakuwa waaminifu kwa BWANA. Wafalme wachache sana wanasifiwa kufanya mema mbele za BWANA. Hata hivyo, hawakufikia kiwango cha Daudi.
Yaliyomo:
1. Mwisho wa maisha ya Daudi na utawala wa Sulemani, Sura 1–2
2. Utawala wa Sulemani, Sura 3–11
3. Mgawanyiko wa kidini na kisiasa, Sura 12–13
4. Hali ya falme mbili, Sura 14–16
5. Manabii Eliya na Elisha, Sura 17–19
6. Mfalme Ahabu, Sura 20:1–22:40
7. Wafalme wa Yuda na Israeli, Sura 22:41-53

Currently Selected:

1 Fal UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in