1 Fal 4
4
Maofisa Tawala wa Sulemani
1Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote. 2Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani, 3#2 Sam 8:16Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe;#4:3 Au, mkumbushi. 4#1 Fal 2:35; 2:27na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani; 5#2 Sam 8:18; 20:26; 15:37; 16:16; 1 Nya 27:33na Azaria mwana wa Nathani alikuwa juu ya maakida; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki wake mfalme. 6#1 Fal 5:14Na Ahishari alikuwa juu ya nyumba; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa juu ya shokoa. 7Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula. 8Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu. 9Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Bethshemeshi na Elon-beth-hanani. 10Mwana wa Hesedi, katika Arubothi; na Soko ilikuwa kwake na nchi yote ya Heferi. 11Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake. 12Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu. 13#Hes 32:41; Kum 3:4Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba. 14Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu. 15Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani. 16Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi. 17Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari. 18Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini. 19#Kum 3:8Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa akida wa pekee katika nchi hiyo.
Utukufu wa Utawala wa Sulemani
20 #
Mwa 22:17; 1 Fal 3:8; Mit 14:28; 1 Sam 30:16; 1 Nya 12:39; Ayu 1:18; Zab 72:3; Mik 4:4; Zek 9:15; Mdo 2:46 Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.
21 #
Mwa 15:18; Kut 23:31; Kum 11:24; Yos 1:4; 2 Nya 9:26; Zab 72:8 Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.
22Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori#4:22 Kori ni kipimo cha Kiebrania cha kadiri ya pipa moja. thelathini za unga mzuri, na kori sitini za ngano, 23na ng’ombe kumi walionona, na ng’ombe ishirini za malisho, na kondoo mia, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona. 24#Mwa 10:19Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote. 25#Kum 33:28,29; Zab 33:12; 144:12-15; Yer 23:6; Mik 4:4; Zek 3:10Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
26 #
Kum 17:16; 1 Fal 10:25,26; 2 Nya 9:25; Zab 20:7 Tena Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa magari yake, na wapandao farasi kumi na mbili elfu. 27Na maakida wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu. 28#Est 8:14; Mik 1:13Shayiri pia na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo, kila mtu kwa kadiri ya kazi yake.
Sifa za Hekima ya Sulemani
29Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30#Mwa 25:6; Ayu 4:21; Mit 2:1; Mdo 7:22Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31#1 Nya 15:19; 6:33Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32#Mit 1:1; Mhu 12:9; Wim 1:1Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. 34#1 Fal 10:1; 2 Nya 9:1Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.
Currently Selected:
1 Fal 4: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.