YouVersion Logo
Search Icon

1 Kor 16:13-24

1 Kor 16:13-24 SUV

Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu); watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha. Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu. Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao. Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao. Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha. Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.