YouVersion Logo
Search Icon

1 Kor 12

12
Karama za Roho
1Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu. 2#Hab 2:18,19Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. 3#Mk 9:39; Mt 7:21; 1 Yoh 4:2,3Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
4 # Rum 12:6-8; Efe 4:4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5#Efe 4:11Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 7#1 Kor 14:26Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10#1 Kor 14:5; Mdo 2:4na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; 11#Rum 12:3; Efe 4:7; 1 Kor 7:7lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
Mwili Mmoja wenye Viungo Vingi
12 # Rum 12:4-5; 1 Kor 10:17 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13#Gal 3:28Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 14Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. 15Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? 16Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo? 17Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? 18Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. 19Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 21Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. 22Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 24Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; 25ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 26Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. 27#Rum 12:5; Efe 5:30Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
28 # Efe 4:11,12 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. 29Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? 30Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? 31#1 Kor 14:1Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.

Currently Selected:

1 Kor 12: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in