1 Nya 16
16
Sanduku la Bwana Lawekwa katika Hema
1 #
2 Sam 6:17-19
Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la BWANA. 3Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.
4Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la BWANA, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, BWANA, Mungu wa Israeli; 5Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; 6nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu.
Daudi Aimba Wimbo wa Shukrani
7 #
2 Sam 23:1
Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru BWANA, kwa mkono wa Asafu na nduguze.
8 #
Zab 105:1; 145:1 Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;
Wajulisheni watu matendo yake.
9 #
Zab 95:1,2; 100:1 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi;
Zitafakarini ajabu zake zote.
10 #
Zab 34:3; Isa 45:25 Jisifuni kwa jina lake takatifu;
Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
11 #
Amo 5:6,14 Mtakeni BWANA na nguvu zake;
Utafuteni uso wake siku zote.
12 #
Zab 103:2; 111:2 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya;
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
13Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake,
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
15Likumbukeni agano lake milele,
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
16 #
Mwa 15:18; 17:2; 26:3; Neh 9:8; Ebr 6:13-18 Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka;
17Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri,
Na Israeli liwe agano la milele.
18Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,
Iwe urithi wenu mliopimiwa;
19 #
Mwa 34:30; Ebr 11:13 Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa;
Naam, watu wachache na wageni ndani yake.
20Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa,
Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
21 #
Mwa 12:17; 20:3; Kut 7:15-18 Hakumwacha mtu awaonee;
Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;
22 #
Zab 105:15; 1 Yoh 2:27 Akisema, Msiwaguse masihi#16:22 Au mtiwa mafuta (taz. 1 Sam. 2:10). wangu,
Wala msiwadhuru nabii zangu.
23 #
Zab 47:1; 96:1 Mwimbieni BWANA, nchi yote;
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
24 #
Isa 12:4
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
25 #
Zab 24:8; 89:6-8; Isa 40:25,26 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26 #
Law 19:4; Zab 115:4-8; Isa 45:20; Yer 10:3; 1 Kor 8:4 Maana miungu yote ya watu si kitu;
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
27 #
Zab 8:1
Heshima na adhama ziko mbele zake;
Nguvu na furaha zipo mahali pake.
28Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
29Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Leteni sadaka, mje mbele zake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
30Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
31 #
Isa 35:10; Lk 2:13; Ufu 14:2 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie;
Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;
32 #
Zab 96:10
Bahari na ivume na vyote viijazavyo;
Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
33Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,
Mbele za BWANA,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
34 #
Zab 106:1; 107:1; 118:1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
35 #
Zab 106:47,48 Nanyi mkaseme,
Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe,
Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
Tulishukuru jina lako takatifu,
Tuzifanyie shangwe sifa zako.
36 #
1 Fal 8:15; Zab 72:18,19; Kum 27:15; Neh 8:6 Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.
Ibada Zarejeshwa tena
37Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la agano la BWANA, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake. 38Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu; 39#1 Nya 21:29; 2 Nya 1:3; 1 Fal 3:4na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya BWANA katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni, 40#Kut 29:38; Hes 28:3ili kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya BWANA, aliyowaamuru Israeli; 41#2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Neh 9:17; Zab 25:10; 33:5; 100:5; Yer 33:11; Yoe 2:13; Lk 6:36; Yak 5:11na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele; 42na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni. 43#2 Sam 6:19,20; Mwa 18:19; Yos 24:15Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake.
Currently Selected:
1 Nya 16: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.