YouVersion Logo
Search Icon

Warumi Utangulizi

Utangulizi
Paulo aliwaandikia watakatifu huko Rumi waraka huu. Wengi wa waumini wa kanisa hili walikuwa ni watu wa Mataifa. Paulo anaanza kwa kueleza kwamba wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Kwa hiyo Wayahudi na watu wa Mataifa hawawezi kudai haki mbele za Mungu, kwa sababu dhambi zao zinafuta haki hiyo. Lakini Mungu, kwa neema yake, anatuhesabia haki tuliyoipoteza kwa dhambi, haki tunayoipata kupitia kwa kumwamini Mwanawe, Yesu Kristo. Kwa njia hii ya kuhesabiwa haki na Mungu katika Mwanawe, tunaweza kuwa washindi katika maisha ya Kikristo. Kisha Paulo anaeleza nafasi ya Wayahudi katika mpango wa Mungu. Anamalizia waraka wake kwa kutoa maonyo kadha wa kadha kuhusu maadili.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Paulo kujitambulisha kwa kanisa la Rumi kwa ajili ya maandalizi ya safari yake, na pia ili kueleza kwa muhtasari msingi wa mafundisho yake.
Mahali
Korintho.
Tarehe
Kama mwaka wa 57 B.K.
Wahusika Wakuu
Mtume Paulo, na waumini wa Rumi.
Wazo Kuu
Mpango wa Mungu wa wokovu na haki kwa wanadamu, kwa Wayahudi na pia watu wa Mataifa, kwa kuwa wote ni wenye dhambi (1:16-17).
Mambo Muhimu
Ufunuo kuhusu adhabu ya Mungu dhidi ya dhambi, na haki ipatikanayo kwa njia ya imani kama msingi wa kuhesabiwa haki.
Mgawanyo
Utangulizi (1:1-17)
Watu wote hawana haki (1:18–3:20)
Haki ipatikanayo kwa kumwamini Kristo (3:21–5:21)
Kushinda dhambi kwa uwezo wa Kristo (6:1–8:39)
Mpango wa Mungu kwa Israeli (9:1–11:36)
Misingi ya maisha ya Kikristo (12:1–15:13)
Mawaidha ya mwisho (15:14–16:27).

Currently Selected:

Warumi Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in