YouVersion Logo
Search Icon

2 Wakorintho Utangulizi

Utangulizi
Ingawa inaonekana kwamba waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wakorintho uliwasaidia, bado mivutano na mashindano yalikuwa yakiendelea. Walimu wa uongo walikuwa wamejiingiza ndani ya kanisa, wakiwa wanapinga na hata kushambulia uadilifu wa Paulo mwenyewe, na mamlaka yake kama mtume. Wengine katika kanisa hawakutaka kutubu. Hivyo Paulo aliamua kutorudi huko hadi tabia zao zibadilike.
Paulo aliandika waraka huu kueleza hisia zake kuhusu wajibu, shauku na majukumu katika ushirika wa Wakorintho, na pia kujibu mashambulizi yaliyokuwa yameelekezwa kwake binafsi kama mtume. Katika kushughulikia matatizo hayo, Paulo alithibitisha mamlaka yake kama mtume.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuthibitisha huduma ya Paulo, na kutetea uwezo wake kama mtume, na pia kuyakataa mafundisho ya uongo katika kanisa la Korintho.
Mahali
Makedonia.
Tarehe
Kati ya 55–57 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tito, Timotheo, na walimu wa uongo.
Wazo Kuu
Maisha binafsi na utumishi wa Paulo: anaorodhesha mambo aliyoyapitia katika maisha yake kama mtumishi wa Kristo.
Mambo Muhimu
Jinsi tunavyoweza kupata ushindi katika mateso, na jinsi neema ya Mungu inavyotenda kazi kuleta mema kutokana na mateso. Paulo pia anatetea utume wake na kuwaonya wasiotii.
Mgawanyo
Salamu na utambulisho, faraja kwa Wakristo (1:1–2:4)
Msamaha kwa wale waliotubu (2:5-17)
Maelekezo kuhusu utumishi wa kweli wa Kikristo (3:1–6:2)
Habari za Paulo mwenyewe (6:3–7:16)
Neema ya utoaji na maelekezo kuhusu changizo (8:1–9:15)
Utetezi wa Paulo kuhusu huduma yake (10:1–11:33)
Maono ya Paulo na mwiba aliokuwa nao (12:1–12:21)
Maonyo ya mwisho, na salamu (13:1-14).

Currently Selected:

2 Wakorintho Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in