Luka 22
22
Mpango wa kumwua Yesu
1 #
Mt 26:1-5; Mk 14:1,2 Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo sikukuu ya Pasaka. 2#Lk 20:19 Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu.
3 #
Mt 26:14-16; Mk 14:10,11 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskarioti, naye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili. #Yn 13:2,27 4Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. 5Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha. 6Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.
Maandalizi ya Pasaka
7 #
Mt 26:17-29; Mk 14:12-25 Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja Pasaka. #Kut 12:18-20 8Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie Pasaka tupate kuila. 9Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? 10Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akiwa amebeba mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. 11Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Kiko wapi chumba cha wageni, nipate kula Pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? 12Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, kimekwisha tayarishwa; andaeni humo. 13#Lk 19:32 Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa Pasaka.
Kuanzishwa kwa chakula cha Bwana
14Na saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 15Akawaambia, Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16#Lk 13:29 kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hadi itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. 17Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; 18Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hadi ufalme wa Mungu utakapokuja. 19#1 Kor 11:23-25; Mdo 27:35 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20#Kut 24:8; Yer 31:31; Zek 9:11 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.] 21#Yn 13:21,22 Lakini, tazama, mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani, 22Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye! 23Wakaanza kuulizana wao kwa wao, ni yupi miongoni mwao atakayelitenda jambo hilo.
Mashindano kuhusu ukubwa
24 #
Mt 18:1; Mk 9:34; Lk 9:46 Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa. 25#Mt 20:25-27; Mk 10:42-44 Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa Wenye fadhili; 26#Mt 23:11; Mk 9:35 lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. 27#Yn 13:12-15 Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye. 28Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. 29#Lk 12:32 Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; 30#Mt 19:28 mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
Yesu atabiri kuhusu Petro kumkana
31 #
Mt 26:31-35; Mk 14:27-31; Yn 13:36-38 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; #2 Kor 2:11; Amo 9:9 32#Yn 17:11,15,20; Zab 51:13 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. 33Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni. 34Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.
Mfuko, mkoba, na upanga
35 #
Mt 10:9-10; Mk 6:8-9; Lk 9:3; 10:4 Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La! 36Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho lake akanunue. 37#Isa 53:12; Lk 22:52 Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake. 38Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi.
Yesu aomba katika mlima wa Mizeituni
39 #
Mt 26:30,36-46; Mk 14:26,32-42 Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye. #Lk 21:37; Yn 18:1
40Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. 41Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, 42#Mt 6:10 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; lakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [ 43#1 Fal 19:5; Yn 12:29 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. 44Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka chini.] 45Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni. 46Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.
Kusalitiwa na kukamatwa kwa Yesu
47 #
Mt 26:47-56; Mk 14:43-49; Yn 18:2-11 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. 48Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? 49Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotokea, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga? 50Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kulia. 51Yesu akajibu akasema, Muwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya. 52#Lk 22:37 Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maofisa wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja mkiwa na panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi? 53#Lk 19:47; 21:37; Yn 7:30; 8:20; Kol 1:13 Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, ya mamlaka ya giza.
Petro amkana Yesu
54 #
Mt 26:57,58,69-75; Mk 14:53,54,66-72; Yn 18:12-18,25-27 Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali. 55Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye Petro akaketi kati yao. 56Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi akiwa katika mwanga, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye. 57Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. 58Muda mfupi baadaye mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi. 59Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikazia akisema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya. 60Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika. 61#Lk 22:34 Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu. 62Akatoka nje akalia kwa majonzi.
Kumdhihaki na kumpiga Yesu
63 #
Mt 26:67,68; Mk 14:65 Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. 64Wakamfunika macho, kisha wakamwulizauliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga? 65Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana.
Yesu mbele ya baraza
66 #
Mt 26:59-66; Mk 14:55-64 Kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema, 67#Yn 3:12; 8:45; 10:24 Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nikiwaambia, hamtasadiki. 68Tena, nikiwauliza, hamtajibu. 69#Dan 7:13; Zab 110:1 Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi. 70Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. 71Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
Цяпер абрана:
Luka 22: RSUVDC
Пазнака
Падзяліцца
Капіяваць
Хочаце, каб вашыя адзнакі былі захаваны на ўсіх вашых прыладах? Зарэгіструйцеся або ўвайдзіце
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.