Mwanzo 5
5
Wazawa wa Adamu
1 #
1 Nya 1:1; Mt 1:1; Lk 3:38; Efe 4:24; Kol 3:10; Mwa 1:27-28 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2#Mt 19:4; Mk 10:6 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3Adamu akaishi miaka mia moja na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. 4Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 5#Mwa 3:19; Ayu 30:23; Zab 49:7-9; 89:48; Rum 5:12; 1 Kor 15:21; Ebr 9:27 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia tisa na thelathini, naye akafa.
6Sethi akaishi miaka mia moja na mitano, akamzaa Enoshi. 7Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 8Siku zote za Sethi ni miaka mia tisa na kumi na miwili, akafa.
9Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 11Siku zote za Enoshi ni miaka mia tisa na mitano, akafa.
12Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arubaini, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 14Siku zote za Kenani ni miaka mia tisa na kumi, akafa.
15Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 17Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
18 #
1 Nya 1:3; Amu 14:15 Yaredi akaishi miaka mia moja na sitini na miwili, akamzaa Henoko. 19Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 20Siku zote za Yaredi ni miaka mia tisa na sitini na miwili, akafa.
21Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22#Mwa 17:1; 2 Fal 20:3; Zab 16:8; Mik 6:8; Mal 2:6; 1 The 2:12 Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 23Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. 24#2 Fal 2:11; Ebr 11:5; Yud 1:14 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
25Methusela akaishi miaka mia moja na themanini na saba, akamzaa Lameki. 26Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 27Siku zote za Methusela ni miaka mia tisa na sitini na tisa, akafa.
28Lameki akaishi miaka mia moja na themanini na miwili, akazaa mwana. 29#Mwa 3:17; 4:11 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA. 30Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia tano na tisini na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 31Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
32Baada ya Nuhu kufikisha umri wa miaka mia tano, aliwazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Currently Selected:
Mwanzo 5: SRUV
Qaqambisa
Share
Copy
Ufuna ukuba iimbalasane zakho zigcinwe kuzo zonke izixhobo zakho? Bhalisela okanye ngena
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.