Akafanya mjeledi kwa kambaa akawatoa wote katika hekalu, na kondoo, na ngʼombe, akamwaga fedha yao wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoem haya: msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.