Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji
Yesu

Yesu

Tamthilia kuhusu maisha ya Yesu Kristo, filamu ya "YESU", imetafsiriwa katika zaidi ya lugha 1,400 tangu kutolewa kwake mwaka wa 1979. Imebakia kuwa filamu iliyotafsiriwa zaidi na iliyotazamwa na watu wengi katika historia. Mchungaji Rick Warren, mwandishi wa "The Purpose Driven Life," anasema "filamu ya 'Yesu' ni chombo cha manufaa zaidi cha kiinjilisti kilichoumbwa."Viongozi wa kidini na wasomi zaidi ya 450 wametathmini hati ili kuhakikisha usahihi wa kihistoria na kibiblia. Hati hii inalingana na injili ya Luka, kwa hivyo karibu kila neno Yesu anazungumza ni kutoka kwenye Biblia. Juhudi kali za kuonyesha tamaduni za Kiyahudi na Kirumi karibu miaka 2000 ilizopita ni pamoja na: nguo zilizofumwa kwa mkono katika rangi 35 tofauti, vyombo vilivyotengenezwa kwa udongo kutumia mbinu za karne ya kwanza, na kuondolewa kwa nguzo za simu na nyaya za umeme katika mandhari ya nchi yao.YESU alirekodiwa kwenye filamu katika maeneo 202 tofauti katika Israeli mwaka wa 1979, pamoja na waisraeli na waarabu takribani zaidi ya 5,000. Ilipowezekana, filamu ilirekodiwa katika maeneo ambayo matukio hayo yalitokea miaka 2,000 iliyopita