Zab 24:1-6
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
Zab 24:1-6