BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye akesha bure.
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema,
Na kukawia kwenda kulala,
Na kula chakula cha taabu;
Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Tazama, wana ndio urithi wa BWANA,
Uzao wa tumbo ni thawabu.