Mit 17:17-28

Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu. Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake. Apendaye ugomvi hupenda dhambi; Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu. Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba. Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe; Wala baba wa mpumbavu hana furaha. Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa. Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu. Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia. Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye, Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa. Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri; Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao. Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara. Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Mit 17:17-28