BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA
Na kumngojea kwa utulivu.
Ni vema mwanadamu aichukue nira
Wakati wa ujana wake.
Na akae peke yake na kunyamaza kimya;
Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.