Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,
Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
Ni mpya kila siku asubuhi;
Uaminifu wako ni mkuu.
BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,
Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.