Wimbo Wa NeemaMfano
Unazisikia kila siku…sauti. Zingine kwenye kichwa chako. Zingine kwenye mitandao ya kijamii. Zingine kutoka kwa marafiki wako. Zingine hutoka kwa wale ambao hukuchukia hadharani.
Ni sauti ambazo zinajaribu kukuambia wewe ni nani… na nini kitachohitajika ili uweze kuwa mtu unayepaswa kuwa.
Tatizo moja na sauti hizo ni kwamba haziwezi kutimiza ahadi zake. Utambulisho wako sio kitu ambacho unastahili, unachotafuta wewe mwenyewe, au unachopigania kuhifadhi. Ni zawadi kutoka kwa Mungu, na ninataka kukusaidia kuitambua leo.
Mchungaji na mwanatheolojia John Piper ameandika, "Katika Yesu, hatupotezi utambulisho wetu wa kweli, lakini tunapata utambulisho wetu, kupitia kwake tu."
Kwa hivyo unapata wapi utambulisho wako wa kweli?
Katika pesa? Katika wafuasi? Katika mafanikio? Katika sura? Katika siasa? Katika mamlaka? Katika hadhi? Katika ngono?
La, kwa Yesu tu.
2 Wakorintho 5:17 inasema, "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya!" (NIV)
Hii ni habari njema! Inamaanishoa hakuna mjadala kuhusu jinsi ulivyo. Utambulisho wako unatoka kwa Mungu aliyekuumba na aliyekuokoa. Anasema, "Wewe ni kiumbe kipya kwa sababu ya Yesu…uko huru kutokana na kujaribu kukubalika na wengine, uko huru kutokana na kujaribu kudhibitisha thamani yako, na huru kutokana na kuikimbia jana yako."
Kwa neema ya Mungu kupitia Yesu, wewe sio kile ambacho ulikuwa zamani, kile ambacho wengine wanakifikiria, au kile ambacho dunia inasema unafaa kuwa. Badala yake, wewe ni mtoto mpendwa wa Mungu.
Na hii ndio habari njema zaidi…
Kwa sababu Mungu alikuumba, kadiri unavyomkaribia, ndivyo unavyoendelea kuwa kiumbe kamili alichokuumba uwe. Kwa namna fulani, Mungu anakurejeshea utambulisho wako, kitu ambacho tunachukua muda na juhudi nyingi kujitafutia.
Je, unajua hilo linamaanisha nini?
Kila wakati wengine wanapokuweka chini, unajiuliza, au unahisi msukumo wa kukubaliwa na dunia, una ukweli wa kushikilia. Unaweza kusimama imara na kusema, " Ninajua mimi ni nani. Hakuna maswali. Mimi ni mtoto wa Mungu, nimesamehewa, nimewekwa huru, na nikaumbwa upya kupitia Yesu."
Jaribu hilo leo: kazini, kwenye mitandao ya kijamii, na marafiki wako, moyoni mwako tu. Jihakikishie ni nani Mungu anasema ni wewe kupitia Yesu. Pokea hilo. Amini hilo. Ishi ndani yake. Na usisahau kamwe jinsi Mungu anavyokupenda sana.
Baraka,
—Nick Hall
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua undani wa upendo wa Mungu kwako kupitia ibada hii ya Wimbo wa Neema. Mwinjilisti Nick Hall atakuongoza kupitia ibada yenye nguvu ya siku 5 akikualika kujiunga na Wimbo wa neema ya Mungu unaoimbwa juu yako.
More
Tungependa kuwashukuru PULSE Outreach kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://anthemofgrace.com/