Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Habari za wajitu (Warefai) tuzinapata mara ya kwanza Mwa 15:20 na baadaye Yos 17:15 na Kumb 2:20-21 (Nchi hiyo nayo yadhaniwa kuwa ni nchi ya Warefai, hapo kale Warefai walikaa humo). Katika m.19 imeandikwa kuwa Elhanani alimwua Goliathi. Je, siye Daudi aliyemwua huyu? Ndiyo! Katika 1 Sam 17:23 na 50 tunasoma kwamba yule shujaa alitokea, ... jina lake Goliathi ... Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua. Ili kutatua utata huu, kumbuka kwamba habari ya m.19 inazungumzia vita tofauti iliyotokea baadaye wakati Daudi alipokuwa mfalme, tena hakuwa na nguvu kama wakati alipokuwa kijana (m.15). Hivyo bila shaka aliyeuawa na Elhanani ni Mrefai mwingine. Hapo habari za 1 Nya 20:5-6 zinaweza kutusaidia. Imeandikwa kwamba huyo aliyeuawa na Elhanani ni ndugu yake Goliathi! Neno latika m.17, Usije ukaizima taa ya Israeli, ni la mfano. Katika nyumba ya Mungu kulikuwa na taa iliyowaka daima kama dalili ya kudumu kwa watu wa Mungu. Watu wa Daudi walimwambia kwamba ikiwa yeye atakufa, basi watu wa Mungu hawataweza kuendelea kuwepo, maana Daudi ndiye mfalme wao. Katika 1 Fal 11:36 imeandikwa kuwa Mungu alihakikishia Daudi apate kuwa na taa siku zote ... katika Yerusalemu, yaani, mtu wa ukoo wa Daudi ataendelea kuwa mfalme. Habari hiyo inatukumbusha Zab 132:17 ilipoandikwa, Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. Yesu ametimiza ahadi hizo kwa ukamilifu. Anasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima (Yn 8:12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/