Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Katika sehemu hii ya Zaburi, Daudi anaendelea kueleza kwa nini anamkiri Bwana kuwa Mungu wake. Ndiye mshauri wa ajabu, maana anamjulisha Daudi njia ya uzima (Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri ... Utanijulisha njia ya uzima; m.7 na 11). Tukifuata shauri la Bwana, linaimarisha uhusiano kati yetu na yeye (yuko kuumeni kwangu, Daudi anashuhudia katika m.8). Pia linajazia maisha yetu furaha na kuletea hata mwili wetu tumaini (m.9, Moyo wangu unafurahi ... mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini). Katika Mdo 2:29-31 twajifunza kwamba Zab 16:10 ni utabiri juu ya kufufuka kwa Bwana Yesu: Yeye mwenyewe [Daudi] akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu. Sisi tukimwamini Yesu, habari hiyo njema ina maana kubwa hata kwetu, kama Daudi anavyosema katika m.11, Utanijulisha njia ya uzima ... katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/