Unayo Maombi!Mfano
“Funguo Sita za Maombi Yenye Afya na Yaliyo Sawa – Sehemu ya Pili”
4. Mwambie Mungu mahitaji yako binafsi na muombe Ayafikie. “Utupe leo riziki yetu…”
Upendo wa Mungu kwako ni wa kina, usio na mwisho na hauna sababu, wakati wote ukilinganishwa kwenye Biblia na huruma za baba aliyejaa upendo kwa mwanaye. Anataka kusikia kutoka mwanae ( wewe); Anataka kusikia juu ya maisha yako, mahitaji yako, shauku zako, na Anataka wewe uende Kwake kwa mahitaji hayo. Upendo wake kwako unamsukuma kuzidi kukubariki zaidi ya unavyoweza kutazamia.
5. Muombe akusamehe makosa yako, ukizingatia hitaji lako la kuwasamehe wengine waliokukosea. “Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.”
Kumuomba Mungu kutusamehe dhambi zetu huanzia kwanza kwa sisi kukubali dhambi zetu, na halafu kuzikiri kwa Mungu.
“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” I Yohana 1:9
Unaweza kujihakikisha kuwa Mungu amekusamehe na kukusafisha kutoka dhambi zako. Katika msamaha huo, pia kuna kuwekwa huru mbali na shutuma, aibu na hukumu.
Lakini pia Mungu anataka kama Alivyotusamehe sisi, nasi tusamehe wengine waliotukosea. Kama vile ambavyo kupokea msamaha toka kwa Mungu kunavyoleta uhuru, vivyo hivyo kuwasamehe wengine – uhuru kutoka uchungu, manung’uniko, na kuruhusu mambo ya nyuma yaliyotuumiza kuendelea kutuumiza.
Msamaha, unaopokea na unaotoa, yote ni muhimu katika kuishi maisha ya uhuru katika Kristo.
6. Omba uongozi wa Mungu kukusaidia kujiepusha na majaribu na hali ambazo hazipendezi Kwake. “…na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na Yule mwovu.”
Mungu ametusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka katika udhalimu wote kama ilivyoahidiwa katika I Yohana 1:9, lakini bado tutakutana na majaribu, tunapoishi katika ulimwengu huu ulioanguka. Sehemu hii ya sala ya Bwana inasisitiza umuhimu wa kutokuwa wavivu na hatimaye kuwa na mashaka na msamaha anaotupatia Mungu, bila ya kukumbuka umuhimu wa kujilinda na dhambi siku za mbele. Ingawa Mungu huondoa adhabu ya kiroho ya dhambi zetu kwa kutusamehe, lakini haondoi matokeo mabaya ya dhambi. Kwa sababu hiyo ni muhimu kuomba msaada wa Mungu wa kutusaidia kuepuka majaribu ya dhambi.
Kila siku, anza kumpa Mungu muda wo wote unaoweza kuutoa kwa furaha Kwake katika maombi. Mungu hana kiwango cha muda alichokuwekea ukifikie kila siku. Zaidi pia, itakuwa changamoto wakati mwingine kuwa macho na “kuzuia kushindwa”. Usikate tamaa; fahamu kwamba utakuwa aliyebarikiwa na Mungu unapojitoa Kwake kwa maombi!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2